Balozi wa Marekani
katika Umoja wa Mataifa Nikki Harley ameapa kuyataja mataifa yanaounga
mkono Korea Kaskazini na mpango wake wa kinyuklia huku hali ya wasiwasi
ikiendelea.
Matamshi yake yanajiri kufuatia mkutano wa dharura wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.
Baraza hilo siku ya Jumatatu kwa pamoja lilishutumu jaribio la kombora la masafa marefu lililotekelezwa na Korea Kaskazini na kuonya kuhusu vikwazo vipya.
Korea kaskazini inesema kuwa kombora hilo lililofanyiwa majaribio ni jipya na lina uwezo wa kubeba kichwa cha kinyuklia.
- Kombora la Korea Kaskazini lashindwa kupaa
- Marekani: Korea Kaskazini ilikusudia uchokozi
- Uwezo wa kijeshi wa Korea Kaskazini
Hatahivyo Korea Kusini ilishindwa kubaini habari hiyo.
Akizungumza katika mkutano wa faragha wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Jumanne , bi Harley aliyaonya mataifa yanayounga mkono Korea Kaskazini kuwacha kauli hiyo la sivyo yaone cha mtema kuni.
''Iwapo wewe ni taifa linalounga mkono Korea Kaskazini tutakutaja.Tutahakikisha kila mtu anajua wewe ni nani na tutakuwekea vikwazo hata wewe '', aliwaambia maripota akiandamana na balozi wa Japan na Korea Kusini katika umoja huo.
Washington alisema, inaunga mkono mazungumzo na Pyongyang iwapo taifa hilo litasitisha majaribio ya makombora ya masafa marefu na yale ya kinyuklia.
SHARE
No comments:
Post a Comment