Rais Donald Trump
alimtaka aliyekuwa mkurugenzi wa shirika la FBI James Comey kusitisha
uchunguzi uliokuwa ukiendelea dhidi ya aliyekuwa mshauri wa maswala ya
usalama Michael Flynn.
''Natumai utawachana na haya'', bwana Trump
aliripotiwa akimwambia Bwana Comey baada ya mkutano katika Ikulu ya
Whitehouse mnamo mwezi Februari kulingana na bahrua ilioandikwa na James
Comey.Barua hiyo iliandikwa mara moja baada ya mkutano, siku moja baada ya Michael Flynn kujiuzulu kulingana na vyombo vya habari vya Marekani.
Ikulu ya Whitehouse imekana ripoti hiyo katika taarifa.
''Rais Trump hajamtaka bwana Comey ama mtu yeyote kusitisha uchunguzi ikiwemo uchunguzi wowote unaohusiana na jenerali Flynn'', ilisema.
Bwana Flynn alilazimika kujiuzulu mnamo mwezi Februari baada ya kumdanganya makamu wa rais kuhusu mazungumzo yake na balozi wa Urusi kabla ya Trump kuchukua mamlaka.
SHARE
No comments:
Post a Comment