Marehemu Paul Sozigwa
ALIYEKUWA Mwandishi Habari wa baba wa taifa Mwalimu Julias Kambarage Nyerere, Paul Sozigwa
amefariki dunia, alipokuwa akipatiwa matibabu kwenye Taasisi ya Moyo
ya Jakaya Kikwete (JKCI).
Mtoto
wa Mzee Sozigwa, Mchungaji Moses Sozigwa alisema tatizo la kwanza
lililokuwa likimsumbua baba yao ni kupoteza kumbukumbu. Baadaye ilikuja
kubainika ana tatizo la moyo, madaktari walisema moyo wake umekuwa
mkubwa. Paul Sozigwa ndiye Katibu wa kwanza wa Rais (IKULU-HABARI).
Mbali
na kuwa katibu wa Ikulu, nyadhifa nyingine alizoshika ni Mkurugenzi wa
kwanza wa Redio Tanzania(RTD), DO Wilaya ya Kisarawe katika serikali ya
kikoloni na katibu Mkuu, Wizara ya Habari na Utangazaji.
Kutoka kushoto: Habib Halala, Paul Sozigwa, Mwalimu J.K. Nyerere, Brig. Hashim Mbita na Benjamin Mkapa mwaka 1985.
Vilevile
alishawahi kushika nafasi mbalimbali ndani ya CCM zikiwemo za Mjumbe wa
NEC, CC na M/kiti Tume ya Taifa ya Udhibiti na Nidhamu na M/kiti wa CCM
mkoa wa Pwani.
SHARE
No comments:
Post a Comment