TRA

TRA

Friday, May 12, 2017

Mlipuko wa kipindupindu waua watu 51 Yemen

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !
Mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu nchini Yemen umesababisha vifo vya watu 51 katika kipindi cha wiki mbili. Hayo ni kulingana na taarifa zilizotolewa jana na Shirika la Afya Duniani, WHO.

Shirika hilo limebaini takriban visa 2,752 vya maambukizi hayo tokea Aprili 27. Tayari WHO imefungua vituo 10 vya tiba katika mji wa Sana'a kujaribu kuyazuia maambukizi hayo kusambaa zaidi.

            Mgonjwa akipatiwa matibabu

 Mwakilishi wa WHO nchini Yemen, Dk. Nevio Zagari, amesema wana wasiwasi mkubwa wa kuibuka kwa maambukizi ya kipindupindu katika maeneo kadhaa ya taifa hilo masikini na lililo kwenye vita, akitoa wito wa juhudi zaidi za kimataifa. 

Mfumo wa afya nchini Yemen umedhoofika baada ya miaka miwili ya vita, na kuharibika kwa miundo mbinu ya usafi wa mazingira kunachangia kuenea kwa vimelea katika vyanzo vya maji.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger