TRA

TRA

Friday, May 12, 2017

Brazil yaondoa tahadhari iliyoweka ya hatari ya virusi vya Zika

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !
Brasilia 
Brazil imeondoa tahadhari iliyoweka miezi 18 iliyopita baada ya virusi vya Zika kusababisha kasoro mbalimbali kwa watoto waliozaliwa. 

Kulingana na wizara ya afya nchini humo, kulikuwa na visa 7,900 pekee vya maambukizi ya Zika kati ya mwezi Januari na Aprili mwaka huu, tofauti na visa 170,000 katika kipindi sawa na hicho mwaka uliopita, ikiwa ni upungufu wa asilimia 95.

Kadhalika idadi ya watoto waliozaliwa wakiwa na ulemavu wa ubongo kutokana na virusi hivyo imepungua.

   Wataalamu wa afya wakinyunyuzi dawa kudhibiti Zika

Hata hivyo, serikali ya nchi hiyo imesema itaendelea na mapambano dhidi ya virusi hivyo. Virusi vya Zika huenezwa na mbu anayesababisha homa ya manjano lakini pia huweza kusambazwa kupitia kitendo cha kujamiana. 

Mnamo mwezi Februari mwaka uliopita, Shirika la Afya Duniani, WHO, lilitangaza hali ya hatari na kuwashauri wanawake katika baadhi ya nchi kutoshika mimba kutokana na hofu ya virusi hivyo vilivyoenea mno katika nchi za Amerika. 

Inakisiwa kuwa zaidi ya raia milioni moja wa Brazil waliambukizwa virusi hivyo.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger