TRA

TRA

Monday, May 15, 2017

MRADI WA “DREAM”WAWANUFAISHA VIJANA MBEYA

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


Meneja wa Kihumbe, Ptolemy Samwel, akizungumza na Waandishi wa habari kuhusiana na Mradi wa DREAM. Wafadhili wa Mradi wa DREAM wakizungumza na baadhi ya vijana walionufaika na mradi wa Dream unaosimamiwa na Kihumbe baada ya kuwatembelea Wafadhili wa Mradi wa DREAM wakiangalia baadhi ya bidhaa mbali mbali walizonufaika nazo vijana wanaoishi katika mazingira magumu Wanufaika wa Mradi wa DREAM wakiwa na bidhaa zao Vijana walionufaika na mradi wa DREAM wakiwa katika picha ya Pamoja na Wafadhili wao.

VIJANA zaidi  970 wanaoishi kwenye mazingira hatarishi jijini Mbeya wamenufaika na mradi wa DREAM ambao unawalenga wasichana wenye umri barehe.
Mradi huo wa kuwawezesha mabinti walio kwenye umri wa barehe na wanawake wanaoishi katika mazingira hatarishi ‘Dream’ unaotekelezwa na Kikundi cha Huduma majumbani mkoani Mbeya (Kihumbe) kwa ufadhili wa Walter Reed Program(WRP).
Akizungumza na wandishi wa Habari kuhusu mradi huo, Meneja wa Kihumbe, Ptolemy Samwel, alisema vijana hao wamenufaika na mradi huo kwa kuwezeshwa masuala ya ujasiriamali na utunzaji wa fedha ili ziwasaidie kuinua kipato.
Alisema vijana hao wamewezeshwa kujiunga na vikundi vya ujasiriamali 50 ndani ya kata zote 36 za Jiji la Mbeya ili waweze kujiendeleza na kukopesheka kirahisi na taasisi za kifedha na kuendeleza shughuli zao.
Alisema wengi wa vijana hao walikuwa wanaishi katika mazingira hatarishi ambayo yangewapelekea kupata maambukizi ya virusi vya ukimwi (VVU) na Ukimwi pamoja na mimba zisizotarajiwa hasa kwa watoto wa kike kutokana na biashara ya ngono.
Kwa upande wake mratibu wa mradi huo wa Dream kutoka kwenye kikundi hicho, Anna Mcharo, alisema mradi huo ulianza mwezi Mei mwaka jana na kwamba vijana hao walikuwa wanapatikana kwa kujaza madodoso maalumu na waliogundulika kuwa na sifa walichukuliwa.
Alisema mradi ulikuwa unawalenga zaidi wasichana na wanawake lakini waliamua kuwaingiza wanaume ambao wengi wao ni wenza wa mabinti kwa ajili ya kutambua kinachofanyika na kuepuka kuibuka kwa unyanyasaji wa kijinsia.
Mchalo alisema vijana hao pia wamefundishwa njia mbalimbali za kuepuka unyanyasaji wa kijinsia, mbinu mbalimbali za uzazi wa mpango, njia za kuepuka maambukizi ya Ukimwi, na madhara ya mimba za utotoni.
Alisema lengo la mradi huo wa Dream ni kuwafikia vijana 7000 ndani ya Jiji la Mbeya kufikia Mwezi mei mwaka 2018 lakini mpaka sasa umewafikia vijana 976 ambao wasichana ni 688 na wavulana 288.
Mmoja wa wasichana walionufaika na mradi huo, Upendo Anyambilile, alisema kabla hajaingia kwenye mradi huo alikuwa anafanya biashara ya ngono wakati akiwa na umri mdogo kutokana na hali ya maisha kuwa ngumu.
Alisema katika biashara hiyo ya ngono alipata mimba isiyotarajiwa na kujifungua lakini mwanaume aliyempa ujauzito huo aliukataa na kumtelekeza jijini Dar Es Salaam mpaka aliposafirishwa na wasamaria wema kurudi Mbeya.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger