Msichana wa miaka
14 aliyejisalimisha alipokuwa akitekeleza shambulio la kujitolea
muhanga katika kambi ya jeshi kaskazini mwa jimbo la Maiduguri nchini
Nigeria amesema aliteuliwa kutekeleza shambulio hilo kwa kukataa kuolewa
na waasi wa Boko Haram.
''Nimesalia kwa zaidi ya miaka mitatu katika mikono ya Boko Haram. Wafuasi watatu tofauti wa kundi hilo waliwasilisha ombi la kutaka kunioa lakini nikakataa.
Wawili kati yao walikuwa makamanda.
Nilipokataa kwa mara ya tatu , kamanda mmoja alikasirika na kunitishia kuniua mimi na babangu.
- Buhari na Wasichana wa Chibok
- Wasichana wa Chibok waungana na familia
- Wasichana wa Chibok walibadilishwa na makamanda
- Wasichana wa Chibok wakutana na makamu wa rais Nigeria
''Baada ya wiki moja , wakasema kwa vile nimekataa kuolewa , ninastahili kupelekwa huko Maiduguri kutekeleza mauaji.Watatu wakanishika mikono yangu na wakanidunga sindano.''
Aliambia shirika la habari la Nigeria (NAM) kwamba baadaye alisafirishwa katika kambi ya jeshi pamoja na washambulizi wengine.
Mmoja wao alilipua bomu lake kwenye mkanda wake wa kifuani , lakini lilimua yeye mwenyewe, kwa upande wake mwengine, alisema alipigwa risasi na wanajeshi, Shirika la habari la Nigeria limeripoti.
Alisema hivyo na akatoa mkanda wake wa bomu na kujisalimisha.
CHANZO: BBC
SHARE
No comments:
Post a Comment