viongozi
wa shirika la LEAT pamoja na viongozi wa kijiji cha Uhambila wakiwa
kwenye mkutano wa hadhara wakati wa kujadili maswala ya utunzaji wa
Maliasili na vyanzo vya maji vilivyopo eneo hill.
Baadhi
ya wananchi wakisikiliza kinachoendelea kwenye mkutano wa kijiji wa
kujadili maswala ya utunzaji wa vyanzo vya maji pamoja Maliasili za
kijiji hicho.
Na Fredy Mgunda, Iringa.
Wananchi
wa kijiji cha uhambila wilayani Mufindi Mkoani Iringa wametakiwa
kutunza na kuvilinda vyanzo vya maji na maliasili zilizopo katika kijiji
hicho.
Akizungumza
wakati wa mkutano wa hadhara wa kijiji hicho Afisa mradi kutoka shirika
la LEAT upande wa wilaya ya mufindi Jamali Juma alisema kuwa wananchi
wanatakiwa kujiepusha na ukataji miti hovyo na kulima vinyungu kwenye
vyanzo vya maji kwa kuwa kufanya hivyo kunasababisha ukame.
“Mkiangalia
zamani maeneo haya yalikuwa ya kijani na tulikuwa na mito midogo midogo
mingi iliyokuwa inatililisha maji msimu mzima lakini hali ya sasa haipo
hivyo kutokana na kutaka miti na kuaharibu vyanzo maji nawaomba
wananchi acheni hiyo tabia ili tuwe na Mazingira mazuri kama
zamani”alisema juma
Ukataji
miti na uharibifu wa vyanzo unasababisha madhara mengi makubwa na ndio
maana tunaona sasa kumekuwa na magonjwa mengi ambayo yanaathari ya moja
kwa moja kwa mwanadamu lakini pia uharibifu huo husababisha mabadiliko
ya vipindi vya mvua na kukosekana kwa mvua za kutosha.
Juma
alisema kuwa dunia kwa sasa inakabiliana na swala la mabadiliko ya tabia
nchi hata hivyo wananchi mnatakiwa kuwa umakini ili msije mkaishi
kwenye jangwa kutokana na uharibifu wetu.
“Ni
kosa la jinai kwa mtu yoyote yule kukata miti bila kibali au kuharibu
vyanzo vya maji kutokana na sheria zetu za mwaka 1982 hivyo kukata miti
au kuaribu vyanzo vya maji sio haki ya msingi ya mwananchi” alisema Juma
Shirika
lisilo la kiserikali la Mwanasheria watetezi wa Mazingira kwa vitendo(
LEAT) wametoa elimu ya Mazingira kwa miaka minne mfululizo hivyo Vijiji
vyote vya mradi ambavyo vipo wilaya ya iringa na wilaya ya Mufindi na
kuiomba serikali kuendelea kuboresha Mazingira ambayo yapo chini yao.
Franklin
Masika ni Afisa ughani wa shirika la LEAT aliwataka wananchi kufuata
sheria ya mazingira mwaka 2004 namba 20 na sheria ya maji ya mwaka 2009
namba 11 zinaeleza wazi kuhusu kilimo cha vinyungu au kulima kandokando
ya mto au kwenye vyanzo vya maji na kuna faini zimeolodhishwa hivyo
sheria hizi sio ngeni ili zilikuwa hazifuatwi lakini saizi serikali
imeanza kuzifuatilia kwa umakini zaidi.
“Mkiangalia
nyie hapa kijiji cha uhambila kipo katika bonde la mto rufiji hivyo
wananchi mnatakiwa kuwa makini na hizi sheria kwa kuwa lengo la serikali
ni kuboresha Mazingira ya kuukuza mto ruaha mkuu ambao unahati hati ya
kutoweka na nyie ni walinzi namba moja wa Mazingira “alisema Masika
Lakini
Franklin Masika aliztaja baadhi ya adhabu zinazotokana na uharibifu wa
Mazingira mfano kuchepusha maji,kukinga,kuchukua au kutumia maji kinyume
cha sheria ni kosa la jinai na adhabu yake ni shilingi 300,000 na
isiyozidi 500,000 au kifungo cha miezi miwili na kifungo kisichozidi
miezi sita au vyote viwili kwa pamoja hivyo wananchi wanapaswa kuwa
makini na hizo sheria.
Masika
aliwataka wananchi wa kijiji cha uhambila kuwa kutunza vyanzo vya maji
na Mazingira kwa ujumla ili kuboresha maeneo wanayoishi na kupunguza au
kufuta Kabisa milipuko ya magonjwa ilanayotokea mara kwa mara katika
maeneo ya Vijijini.
Chelsoni
Kikoti, Amani Nyakunga na Reginandi Chalamila ni wananchi wa kijiji cha
uhambila waliiomba serikali zitafakali upya sheria hizo kwa kuwa
zinawaumiza wananchi wa vijijini kutokana na Mazingira wanayoishi
kutokuwa rafiki na namna ya kupata kipato hivyo wemekuwa wakitegemea
sana kilimo cha mboga mboga kuendesha maisha yao.
“Hebu
angalieni Mazingira haya tunayoishi hakuna njia nyingine ya kupata
kipato zaidi ya kutegemea kulima vinyunguni ambako tunalima mboga mboga
tu jamani hee tuatakufa na njaa hebu muishauri serikali juu sheria
hizo”walisema wananchi
Thomas
Mtelega afisana mradi wataasisi ya mufindi kwa maendeleo (MUVIMA)
aliwaomba wananchi kulima Kilimo cha kisasa kutokana na Mazingira
wanayoishi na kuacha tabia za kukata miti pamoja na kuharibu vyanzo vya
maji mfano kulima mboga mboga ni rahisi unaweza kulima hata kwa kutumia
maji.
“Kuna
maji machafu ambayo tunayoyatumia majumbani kwetu ni maji ambayo
tunaweza kuyatumia katika Kilimo cha mboga mboga kwa kuchukua udongo na
kuuweka kwenye gunia au visarufeti ambavyo ukipanda mbegu unaweza kupata
mboga nzuri na salama kwa kuwa guni au kisarufeti kinaweza kujchuja
uchafu wote na kuiacha mboga ikiwa salama hivyo nawashauri wananchi
kutumia njia hii ili kuondokana na ulimaji wa karibu na vyanzo vya maji
na kusababisha Mazingira yanaboresha na kuwa mazuri”alisema Mtelega
Naye
Mwenyekiti wa kijiji cha uhambila Agnes Simba aliwashukuru shirika la
LEAT kwa elimu waliyokuwa wanantoa kwa miaka nne ambayo imewakomboa
wananchi kwa kupata vitu vingi ambavyo sasa vimeanza kutokea na vinakuwa
sio vigeni hasa maswala ya sheria za Maliasili na utunzaji wa vyanzo
vya maji ambavyo vinafaida kwa wananchi wa sasa na baadae.
SHARE
No comments:
Post a Comment