Mmoja wa wasichana
wa Chibok waliotekwa na wapiganaji wa Boko Haram nchini Nigeria ameamua
kusalia na mumewe badala ya kuachiliwa huru kulingana na msemaji wa rais
wa Nigeria.
Alitarajiwa kuwa miongoni mwa kundi la wasichana walioachiliwa siku ya Jumamosi.Garba Shehu aliambia runinga moja kwamba wasichana 83 walitarajiwa kuachiliwa huru lakini mmoja wao akasema : hapana nafurahi nilipo, nimepata mume.
- Buhari na Wasichana wa Chibok
- Wasichana wa Chibok waungana na familia
- Video 'yaonyesha wasichana wa Chibok waliotoweka'
Serikali ilikubali kuwaachilia huru wanachama wanne wa Boko haram kubadilishana na uhuru wa wasichana hao duru ziliambia BBC.
Wapganaji hao wanadaiwa kuwazuilia zaidi ya wasichana 100 kati ya 276 waliowateka katika eneo la Chibok miaka mitatu iliopita.
Kundi hilo pia limewateka maelfu ya raia wakati wa operesheni zao katika eneo hilo.
Inaaminika kwamba baadhi ya wale waliotekwa wameozwa wapiganaji na wamepata watoto nao.
CHANZO: BBC
SHARE
No comments:
Post a Comment