Ofisa Uhusiano wa Selcom, Sabrina Muniru akimuelekeza
namna ya kufanya miamala kupitia mashine ya Selcom, kampuni hizo zimeingia
makubaliano yatakayo wawezesha wateja wa Halopesa kufanya miamala ya kifedha
kupitia mawakala wa selcom nchi nzima.
KATIKA
kufanikisha azma ya kupanua wigo wa huduma za kifedha kwa wananchi wenye vipato
tofauti, kampuni ya mawasiliano ya Halotel imeendelea kuunganisha huduma yake
ya Halopesa na huduma nyingine zaidi ili kuendelea kurahisisha upatikanaji wa
huduma za kifedha kwa Watanzania .
Katika
kulifanikisha hilo Halotel imeingia makubaliano ya mkataba wa utoaji wa huduma na
kampuni ya Selcom, ushirikiano utakaowawezesha mamilioni ya wateja wa mtandao
huo kutoa na kutuma pesa, kununua vocha za muda wa maongezi na kufanya manunuzi
mbalimbali.
Hatua hii
itawawezesha watanzania wengi zaidi kufikiwa na huduma za kifedha kwa njia ya
mtandao ikiwa ni sehemu ya kufanikisha azma ya serikali ambayo inazitaka
taasisi mbalimbali za kifedha kuwafikia wananchi na huduma zao hasa kwa maeneo
ya vijijini.
Akizungumza
wakati wa makubaliano hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halotel, Bw. Le Van Dai
amesema kuwa ni hatua nyingine kubwa katika utoaji wa huduma za kifedha kupitia
simu za mkononi nchini Tanzania. Sasa kupitia huduma ya Halopesa itakuwa imewezesha
kupanua wigo kwa wateja wa mtandao huo kuweza, kutoa na kuweka fedha, pamoja na
kufanya malipo mbalimbali kwa urahisi zaidi.
“Ushirikiano
huu ni wa kipekee katika kurahisisha maisha ya watanzania ambao wamekuwa
wakipata tabu kupata huduma za kifedha kutokana na maeneo wanayoishi. Sisi kama
Halotel hadi sasa tumewafikia watanzania kwa zaidi ya asilimia 95. Hivyo ni
dhahiri kwamba wateja watakaojiunga nasi wataweza kutoa au kuweka fedha huko
huko waliko kupitia kwa mawakala wetu ambao wameenea nchi nzima,” alisema Dai.
“Tunatambua changamoto ambazo kwa
kiasi kikubwa zimekuwa zikiwasibu Watanzania hasa wa kipato cha chini. Kwani
wengi wao walikuwa wanakwama kuweza kupata huduma za kifedha kutokana na
miundombinu kutowafikia. Mpaka hivi sasa Halotel ina mawakala zaidi ya 30,000
walioenea nchi nzima. Hii itawawezesha wakazi wa maeneo ambayo hayakuwahi kuwa
na mawasiliano kabisa au huduma za kibenki sasa kuweza kupata huduma za kifedha
kupitia simu zao za mkononi huko huko walipo,” alihitimisha Mkurugenzi huyo.
Vilevile wateja wa Halopesa
wataweza kutoa na kuweka fedha kwenye akaunti zao za Halopesa kupitia mawakala
wa Selcom zaidi ya 17,000 wanaopatikana nchi nzima.
SHARE
No comments:
Post a Comment