TRA

TRA

Saturday, May 13, 2017

Muhimbili Kuanza Upandikizaji wa Vifaa vya Usikivu Juni, Mwaka Huu

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


mub1
Daktari Bingwa wa Masikio, Pua na Koo, wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Edwin Liyombo akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu huduma ya upandikizaji wa vifaa vya usikivu kwa watoto wenye matatizo ya masikio. Kutoka kushoto ni Maneja wa Bidhaa, Shalini Srivatsan wa Kampuni ya Vanguard (T) Limited na Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Nitesh Patel.
mub2
Baadhi ya wazazi wenye watoto ambao wana matatizo ya usikivu wakimsikiliza Dk. Liyombo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
mub3
Shalini Srivatsan wa Kampuni ya Vanguard (T) Limited akizungumza kwenye  mkutano huo leo.
mub4
Watoto wenye matatizo ya usikivu wakiwa kwenye mkutano huo leo.
mub5
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Wateja wa Hospitali ya Muhimbili, Aminiel Aligaesha (kulia), Mkurugenzi wa Kampuni ya Vanguard (T) Limited, Nitesh Patel na Maneja wa Bidhaa wa kampuni hiyo, Shalini Srivatsan (kushoto) wakimsikiliza Dk Liyombo wa Muhimbili kabla ya kuanza kwa mkutano na waandishi wa habari wakiwamo wazazi wa watoto wenye matatizo ya usikivu. 
…………………………………………………………………….
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo imesema kwamba huduma ya kupandikiza vifaa vya usikivu kwa watoto wenye matatizo ya masikio na watu wengine itaanza kutolewa Juni, mwaka huu.
Huduma ya upandikizaji huo utaipunguzia serikali gharama za kuwapeleka wagonjwa wenye matatizo hayo nchini India.
Kauli hiyo imetolewa leo na Daktari Bingwa wa Masikio, Pua na Koo katika Hospitali ya Muhimbili, Edwan Liyombo wakati wa kutoa elimu kwa wazazi wa watoto wenye matatizo ya masikio jinsi ya kutunza vifaa vya usikivu kwa watoto waliopatiwa huduma hiyo.
Dk Liyombo amesema kwamba huduma itaanza kutolewa nwezi Juni, mwaka huu na kwamba Hospitali ya Muhimbili imeboresha miundombinu na tayari imenunua vifaa kwa ajili ya kuanza kwa huduma hiyo.
Kuhusu gharama za mtoto mmoja kuwekewa kifaa cha usikivu amesema ni ndogo kuliko akiachwa bila kupatiwa huduma hiyo kwani maisha yake yote atakuwa hasikii wala hataweza kupata uelewa wa masomo shuleni.
“Sisi tunaona hakuna gharama ya mtoto kuwekewa kifaa cha usikivu kwa sababu huduma hii ataitumia katika maisha yake yote na akipelekwa shule atakuwa na uwezo wa kusikia na kuzungumza, kwa kifupi atakuwa sawa kama watoto wengine ambao hawana matatizo ya kusikia,” amesema Dk Liyombo.
Akizungumzia lengo la kuwaita wazazi wa watoto wenye matatizo ya kutokusikia, Dk Liyombo amesema ni kuwaelekeza jinsi ya kutunza vifaa hivyo na endapo vina matatizo wanapaswa kutoa taarifa ili virekebishwe.
Amewataka wazazi wenye watoto wenye matatizo ya kusikia kuwapeleka katika hospitali hiyo kwa ajili ya kupatiwa huduma na pia amewataka kinamama wajawazito kuudhuria kliniki ili kuchunguzwa afya zao pamoja na mtoto kwa lengo la kuzuia mtoto kuzaliwa na tatizo la usikivu.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger