Kwa kipindi kizima cha mwezi wa 5
(Mei) wateja wa DStv wamekuwa wakifurahia zaidi vipindi vyenye ubora na
vya kusisimua vya Kiafrika.
Huba, Jikoni na Marion, Mchikicho
wa Pwani, Yahusu Tanzania, Kimbembe ni kati ya vipindi kutoka Tanzania
vilivyo bamba mwezi huu ndani ya chaneli Maisha Magic Bongo (DStv 160).
Meneja Mahusiano Multichoice
Tanzania, Johnson Mshana amesema, “Mwezi Mei kwetu tumeufanya kuwa mwezi
maalum kwa ajili ya kutangaza na kujivunia utajiri wetu waafrika
ikiwa ni pamoja na utamaduni na Sanaa na michezo.
Hii ni moja ya sehemu ya ahadi ya
DStv kwa kutoa ushirikiano kwenye sekta ya sanaa na burudani kwa
kuendelea kusaidia Filamu za Afrika na kwa kuwekeza katika watu, mawazo
na vipaji.
Ikiwa ni njia moja wapo ya
kusheherekea mwezi huu wa Afrka, Wafanyakazi wa Multichoice Tanzania
waliamua kuvaa mavazi maalum ya Kiafrika na kuandaa chakula maalum cha
kiafrika kwa wafanyakazi wote.
Haikuishia hapo, Multichoice
Tanzania pia imeandaa zawadi maalum za Kiafrika kwa waandishi wa habari,
ikiwa ni njia ya kuonyesha shukrani kwa waandishi na kudumisha Umoja na
Uafrika wetu.
SHARE
No comments:
Post a Comment