Mshambuliaji wa timu ya soka ya
Yanga,Donald Ngoma amerejea nchini akitokea nchini Afrika ya Kusini
ambako alikwenda kwa ajili ya matibabu.
Uongozi wa Yanga ulichukua jukumu
la kumpeleka mchezaji huyo kutibiwa nchini Afrika ya Kusini baada ya
kukumbwa na majeraha ya mara kwa mara ambayo yalishindwa kumpa nafasi ya
kucheza vizuri tangu mwezi wa kwanza mwaka huu.
Taarifa zilizopo ni kwamba baada
ya kurejea hapa nchini itamchukua miezi mitatu mchezaji huyo ili kupona
kabisa na kuanza kuitumikia timu hiyo ya Yanga.
Aidha katika hatua nyingine Ngoma
alisema kwamba kwa sasa yeye yupo tayari kuitumikia klabu hiyo msimu
mwingine mmoja baada ya mkataba wake wa awali kuelekea ukiongoni kwa
madai ya kutaka kulipa fadhila kwa klabu hiyo.
Hata hivyo ameshangazwa na taarifa
zinazoeleza kuwa yeye amesaini klabu ya Simba akidai kuwa hakuna kitu
kama hicho na amedai kuwa hawezi kucheza timu nyingine hapa nchini zaidi
ya Yanga hivyo anaamini ikishindindikana ni bora arejee katika timu
yake ya zamani ya FC Platnum.
SHARE
No comments:
Post a Comment