Na Mwandishi Wetu
Wadhamini wa kuu wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara,Kampuni ya
mawasiliano ya Vodacom Tanzania PLC inatarajia kutoa zawadi kwa washindi
wa ligi kuu ya Tanzania Bara kwa msimu wa 2016/2017 siku ya Jumatano.
Pamoja na kutoa zawadi mbali mbali kwa
timu washiriki, kampuni hiyo ambayo ni mdhamini mkuu wa ligi,
imezipongeza timu zote zilizoshiriki msimu huu wa ligi na itatoa zawadi
kwa timu ambazo zimefanikiwa kushika nafasi ya kwanza hadi ya tatu.
Meneja uhusiano wa kampuni hiyo Matina Nkurlu aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuwa, kampuni ya Vodacom inafurahi kuona msimu wa ligi ukimalizika kwa mafanikio makubwa huku timu ya Yanga ikiweza kuibuka mshindi kwa miaka miwili mfululizo.
“Tunaipongeza timu ya Yanga pamoja na mshindi wa pili na wa tatu,Ligi ilikuwa na msisimko pamoja na ushindani mkubwa,” alisema.
Nkurlu aliongeza, “waswahili husema
chanda chema huvishwa pete, tunapenda kuwatangazia wadau wa soka na timu
zilizoshiriki ligi kuu kuwa tarehe 24 siku ya Jumatano tutakuwa na
sherehe kubwa itakayofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani city
ya kukabidhi zawadi yao mabingwa.
Pamoja na mabingwa, timu nyingine
zilizoshiriki zitaweza kuzawadiwa zawadi mbali mbali kwa kuwa zawadi zao
zipo tayari pia kamati Maalum iliyoundwa kusimamia tuzo hizi imefanya
mabadiliko kiasi kwa kuongeza baadhi ya tuzo ambazo hazikuwepo msimu
uliopita lengo ikiwa ni kuboresha tuzo hizi.
Tuzo zilizoongezwa ni: Tuzo ya Heshima
(ambayo itatolewa kwa mwanasoka nguli wa zamani mwenye historia nzuri
kwa soka la Tanzania).”
Alisema Vodacom Tanzania mwaka huu imetoa zawadi mapema kwa kuwa ni utaratibu wa kawaida kwa kampuni hiyo kukabidhi zawadi mara tu baada ya msimu wa ligi kwisha.
“Uchelewaji wa kutoa zawadi hutokana na sababu mbali mbali ambazo zinakuwaga nje ya uwezo wao ikiwamo baadhi ya timu kuwa zinashiriki mashindano mengine kama Kombe la Shirikisho Barani Afrika. Sababu nyingine ni pamoja na mfungo wa mwezi mtuku wa Ramadhani,” alieleza Meneja Uhusiano huyo.
Nkurlu alisema utoaji wa zawadi mapema pia utazisaidia timu kuwa na muda wa kutosha kwa ajili ya kujiandaa na msimu ujao.
SHARE
No comments:
Post a Comment