NA
K-VIS BLOG/N Mashirika ya Habari
POLISI
wa Uingereza wanasema, wanamshikilia kijana mwenye umri wa miaka 23, kuhusiana
na tukio la mlipuko wa bomu lililoua watu 23 pamoja na mlipuaji katika
shambulio la “kigaidi” lililotekelezwa usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa
burudani ambapo mwanamuziki wa Pop kutoka Marekani Arian Grande alikuwa
akitumbuiza mjini Mancester nchini Uingereza.
“Kikundi
cha waislamu wenye msimamo mkali cha Islamic State (IS) kimetangaza kuhusika na
shambulio hilo. “Tunaweza kuthibitisha kuwa tunamshikilia kijana wa miaka 23
kusini mwa Manchester” Polisi wa Manchester wamesema kwenye mtandao wa Twitter
leo Jumanne Mei 23, 2017.
Bomu
la kienyeji lililipuka Jumatatu usiku mwishoni mwa onesho la muziki wakati maelfu
ya watu wengi wao vijana, walikuwa wakihudhuria burudani ya muziki kwenye
ukumbi wa burudani wa Manchester Kaskazini mwa Uingereza, Polisi wamesema.
SHARE
No comments:
Post a Comment