JESHI la Polisi mkoani Dodoma limewatahadharisha wanafunzi wakiwemo wa
vyuo vikuu wanaofanya biashara ya dawa za kulevya na wanaotumia dawa
hizo kuwa hawatakuwa salama kwani wamejipanga kukabiliana na biashara
hiyo.
Kauli hiyo imekuja kufuatia kukamatwa kwa mwanafunzi wa uuguzi katika
Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM). Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro
Mambosasa amesema jana kuwa, jeshi hilo halitaacha kuwachukulia hatua,
wote wanaojihusisha na dawa hizo. “Tutashirikisha vyombo vyote vya
ulinzi na usalama, tutawafuatilia wanafunzi na wasambazaji, popote
walipo hawatakuwa salama,” alisema.
Aliwataka wanafunzi kuzingatia masomo na si kujiingiza kwenye biashara
na matumizi ya dawa za kulevya. Kamanda Mambosasa aliwataka wanafunzi
wenye taarifa za wanaofanya biashara hiyo au kutumia dawa hizo kutoa
taarifa ili waweze kukamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
“Mwanafunzi kaenda shuleni kusoma lakini anauza bangi ili aharibu akili
za wenzake, tunaendelea kuwabaini wanaojihusisha na usambazaji na
utumiaji dawa za kulevya,” alisema.
Alisema jeshi hilo halitaacha kuwachukulia hatua wote wanaojihusisha na
biashara hiyo. Mei 9 mwaka huu, mwanafunzi wa mwaka wa nne wa kozi ya
Uuguzi katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Nelson Matee (24) alikamatwa
na Jeshi la Polisi akiwa na misokoto 826 ya bangi yenye uzito wa
kilogramu 2.8
SHARE
No comments:
Post a Comment