Wataoto wa maeneo ya Nyarugusu
Wilaya ya Mjini,Unguja wakimuangalia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani ) wakati
alipofika katika shehia ya Nyarugusu, Jimbo la Pangawe kuwafariji na
kutoa pole kwa wananchi walioathirika na Nyumba zao zilizobomoka
kutokana na Upepo mkali uliotokea jana katika maeneo yao na kupelekea
uharibifu kwa kung’oka mapaa ya Nyumba wanazoishi, wakati alipofanya
ziara maalum leo,[Picha na Ikulu.]16/05/2017.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatana na Mkuu
wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe,Ayoub Mohamed Mahmoud (mbele) wakati
alipofika katika shehia ya Nyarugusu, Jimbo la Pangawe leo alipofanya
ziara maalum ya kuwafariji wananchi ambao Nyumba zao zimepata athari ya
kun’goka kwa mapaa kutokana na Upepo mkali uliosabisha na
uharibifu huo jana, ambao umepelekea kukosa pahala pa kuishi,[Picha
na Ikulu.]16/05/2017.
Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
(kulia) alipokuwa akisalimiana na Vijana waliojitolea kutoa msaada kwa
Wananchi wa Shehia ya Nyarugusu Jimbo la Pangawe waliopatwa na maafa ya
Nyumba zao kungoka Mapaa kutokana na Upepo Mkali uliotokea jana,
alipofanya ziara maalum ya kuwafariji wananchi hao leo alipofika kutoa
mkono wa pole, [Picha na Ikulu.]16/05/2017.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akizungumza
na kuwasalimia Wananchi wa Shehia ya Nyarugusu Jimbo la Pangawe
waliopatwa na maafa ya Nyumba zao kung’oka Mapaa kutokana na Upepo
Mkali uliotokea jana, alipofika kuwafariji na kuwapa pole kutokana
mtihani walioupata,alipokuwa katika ziara maalum leo akiwa na Viongozi
mbali mbali wa Jimbo hilo, [Picha na Ikulu.]16/05/2017.
Miongoni
mwa Nyumba zilizoharibika kutokana na Upepo Mkali ulitokea jana katika
maeneo ya Nyarugusu Jimbo la Pangawe Mkoa wa Mjini Magharibi na
kupelekea Wananchi kukosa maakaazi ya kuishi,hali hilo aliiyona Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
(hayupo pichani ) wakati alipofanya ziara maalum leo katika Shehia hiyo,
[Picha na Ikulu.]16/05/2017.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa tatu kulia) alipokuwa
akizungumza na kuwasalimia Wananchi wa Shehia ya Nyarugusu Jimbo la
Pangawe waliopatwa na maafa ya Nyumba zao kung’oka Mapaa kutokana na
Upepo Mkali uliotokea jana, alipofika kuwafariji na kuwapa pole
kutokana mtihani walioupata,wakati alipofanya ziara maalum leo akiwa na
Viongozi mbali mbali wa Jimbo hilo, [Picha na Ikulu.]16/05/2017.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) alipokuwa
akisalimiana na Nd,Abdalla Ali Mohamed Mwananchi wa Makondeko Wilaya ya
Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja wakati alipofika Nyumbani kwake
akiwa ni miongoni mwa Wananchi waliopatwa na maafa ya Nyumba zao
kungoka Mapaa kutokana na Upepo Mkali uliotokea jana,Rais alifika katika
shehia hiyo leo wakati alipofanya ziara maalum ya kuwafariji Wananchi,
na kutoa mkono wa pole,(katikati) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi
Mhe,Ayoub Mohamed Mahmoud, [Picha na Ikulu.]16/05/2017.
……………………………………………………………………………..
Na Miza Kona-Maelezo -Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwnyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein amesema Jamii ina wajibu wa kusaidiana pale yanapotokea matukio ya maafa ili kuweza kunusuru matatizo zaidi yanayoweza kujitokeza.
Amesema yanapotokea matukio ya maafa katika Jamii si muda muafaka wa kulaumiana bali ni muda wa jamii kushirikiana kikamilifu na Wahanga kwa kuwasaidia kwa hali na mali.
Rais Shein ameyasema hayo huko katika Shehia ya Pangawe alipotembelea na kuwafariji Wananchi waliopata maafa ya nyumba zao kutokana na upepo mkali uliotokea hapo jana.
Amesema maafa na matukio kama hayo hayaji kwa taarifa yoyote bali ni mipango ya Mungu na kuwataka wananchi waliopatwa na maafa hayo waendelee kuwa na subira.
“Simanzi kubwa imetokea katika Mwezi wa Aprili na Mei kwa kunyesha mvua kubwa ambazo zilileta maafa huko Pemba na upepo mkubwa uliovuma jana ambao umeleta maafa makubwa kwa wananchi kukosa makaazi” alieleza Dkt Shein
Amesema matukio makubwa ya maafa hutokea katika kipindi cha mvua za masika kwani kipindi hicho mvua hunyesha kubwa ambazo hupelekea kuathiri jamii.
“Tusilaumiane, tusiwabeze, tusiwacheke matukio haya yanaweza kumpata mtu yoyote, wakati wowote haya yote yamepangwa na Mungu,wananchi tusaidiane aliyenacho amsaidie mwenziwe” amesisitiza Dkt Shein.
Hata hivyo Dkt Sheim amesema Serikali ina jukumu la msingi la kuwatakia mema wananchi wake kwa kuwasaidia pale wanapopata matatizo na kuwaletea maendeleo kwa kuwapatia misada mbalimbali inayohitajika.
Aidha amewashukuru wananchi kwa ushirikiano wa pamoja na uvumilivu waliokuwa nao kwa kuweza kusaidiana katika maafa hayo yaliyotokea.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud amesema kutokana matukio yaliyotokea jana tayari Serikali imeunda Timu ya wataalamu 15 kutoka Baraza la Manispaa kupita nyumba hadi nyumba kutathmini athari zilizotokea ili kutoa misaada inayohitajika kwa jamii.
Mapema Mbunge wa Jimba la Pangawe Shamsi Vuai Nahodha amewataka wananchi waliopata maafa kuwa na moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu hivyo serikali kushirikiana na viongozi inachukua juhudi kubwa za kuweza kusaidia wananchi walioathirika.
Upepo huo ulitokea jana majira ya saa 3.15 asubuhi ambao jumla ya nyumba 123 ziliathirika na upepo huo.
Miongoni mwa nyumba hizo shehia ya Kinuni nyumba 96,Shehia ya Mwanakwerekwe nyumba 26 na Pangawe nyumba 1.

SHARE
No comments:
Post a Comment