Na Tiganya Vincent-Tabora
19.5.2017
Mkuu
wa Mkoa Bw. Aggrey Mwanri ametoa wito kwa wadau ,Mashirika ya Kimataifa
na Umoja wa Mataifa kuunga mkono juhudi za Serikali ya Tanzania katika
kuhakikisha Watanzania wapya waliopewa uraia wa nchi hii wanapata elimu
ya uraia ili wajue nini maana ya kuwa raia wa Tanzania na hatimaye
waweze kuishi kwa kuzingatia sheria na taratibu za nchi.
Bw. Mwanri alisema hayo jana mjini Tabora wakati alipokutana na Ujumbe wa Mabalozi wa Umoja wa Ulaya walikuwa kwenye ziara
ya kutembelea maeneo mbalimbali na Ulyankulu ili kuangalia jinsi
wanavyoweza kusaidia katika zoezi kuwaunganisha raia hao wapya na raia
wengine.
Aggrey Mwanri
Alisema
kuwa Watanzania hao wapya hajui nini maana ya kuwa raia , hivyo ni vema
wakaelimishwa kuhusu Katiba na Sheria mbalimbali zinatumika hapa nchini
ambazo nao wanatakiwa kuzifuata na kuzitii kama wanavyofanya raia
wengine.
Bw.
Mwanri alisema kuwa elimu hiyo itasaidi kuwaunganisha raia hapo wapya
na wengine ili waweze kuishi vizuri kwa kutii na kuheshimu Sheria za
Tanzania na kujiona wao sio tena wakimbizi bali ni raia.
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa aliongeza amekuwa akiwasisitiza Watanzania hao wapya kuishi nchini kama walivyo Watanzania wengine na sio kuishi kama wanavyotaka wao au kwa taratibu za nchi nyingine.
Bw.
Mwanri alisema kuwa amekuwa akiwaeleza wazi kuwa mtu yoyote aliyepata
bahati ya kupata uraia wa nchi hii akitumia bahati hiyo vibaya na
kusababisha uvunjifu wa sheria za nchini atakuwa anajiondelea ya sifa ya
kuendelea kuwa Mtanzania na hivyo ataishauri Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi kwa ajili kuangalia uwezekazo kufuta uraia wake .
Katika
hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Tabora aliwaeleza mabalozi hao kuwa
Makazi hayo yanakabiliwa na uhaba wa huduma za jamii kama vile maji,
afya na miundombinu.
Kwa
upande wa Balozi wa Umoja wa Ulaya hapa nchini Mhe.Roeland van de Geer
alisema kuwa baada ya kujionea mazingira ya Makazi ya Ulyunkulu wao kama
Umoja wa Ulaya wataenda kujipanga kwa ajili kuangalia ni eneo gani
wanaweza kusaidia kwa ajili ya kupunguza matatizo yanayowakabili
Watanzania hao wapya.
SHARE









No comments:
Post a Comment