Kampuni kubwa ya
mawasiliano ya MTN tawi la Rwanda imetozwa faini ya zaidi ya dolla
milioni 8 za Marekani kwa kile kilichotajwa kuwa kukiuka makubaliano
baina yake na serikali ya nchi hiyo.
Tangazo hilo linasema kuwa MTN ilikwenda kinyume na makubaliano baina yake na serikali na masharti kadhaa waliyotia saini kabla ya kupata leseni ya kufanyia kazi nchini humo
Mamlaka hayo yameishtumu kampuni ya MTN kufunja mkataba na upande wa tatu nje ya nchi kuhusu kuhifadhi data za mawasiliano za kampuni hiyo.
Hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa isipokuwa taarifa kuwa hifadhi ya data hizo inapatikana nchini Uganda ikitumiwa na nchi za maeneo ya afrika ya kati na kusini.
Kwa upande mwingine, tangazo kutoka makao makuu ya MTN nchini Afrika kusini limeeleza kufahamishwa kuhusu faini hiyo na kwamba wataitafakari na kuendelea na mazungumzo na serikali ya Rwanda kuhusu tatizo hilo.
Hii ndiyo faini kubwa zaidi kuwahi kutolewa na mamlaka ya udhibiti wa huduma za umma nchini Rwanda.
Hii ndiyo iliyokuwa kampuni ya kwanza ya mawasilianonchini Rwanda iliyoanza shughuli zake mwaka 1998 na ambayo sasa ina wateja zaidi ya milioni 4 .
CHANZO: BBC
SHARE









No comments:
Post a Comment