Waziri wa Afya ,Maendeleo
yajamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiongea mbele ya waandishi
wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu hatua zilizochukuliwa na
Serikali katika kujikinga na Ugonjwa wa Ebola uliopo nchini Congo ili
usiingie Tanzania.
…………………………
Na Ally Daud-WAMJW DAR ES SALAAM
SERIKALI imeongeza mashine nne za
kupimia virusi vya ugonjwa wa Ebola katika mipaka ya
Holoholo,Mutukula,Rusumo na Silali ili kudhibiti na kutambua hali ya
maambukizi ya ugonjwa huo kwa wasafiri wa ndani na nje ya Tanzania.
Akizungumza hayo wakati wa mkutano
na waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema
kuwa hatua mbalimbali zinachukuliwa kuhusu kujikinga na ugonjwa huo
usiingie nchini.
“Moja ya hatua tuliyochukua kama
Wizara ya Afya ni kuweka mfumo wa kufuatilia magonjwa (Intergreted
Disease available system) na kujua taarifa za wasafiri katika mipaka
yote kwa wanaotoka nchini Congo kuingia Tanzania ili kujua wanapotoka
mpaka wanapofikia hakuna maambukizi ya ebola “ alisema Waziri Ummy.
Aidha Waziri Ummy amesema kuwa
mbali na hatua hizo Serikali imegawa vifaa vya kujikinga na maambukizi
ya Ebola ikiwemo gauni la kujikinga,mawani,mabuti pamoja na vidonge vya
Chroline katika mipaka yote ili kuzuia maambukizi ya ugonjwa huo kwa
watumishi wanaofanya kazi mipakani.
Kwa mujibu wa Waziri Ummy amesema
kuwa wanaendelea kutoa elimu kwa kuweka mabango yanayohusu ebola katika
mipaka yote na vituo vya kusafiria ikiwemo viwanja vya Ndege,Bandari na
vituo vya mipakani na kupitia njia ya simu kwa kupiga namba 117 kwa
mitandao yote.
“Hakuna mtu aliyethibitishwa kuwa
na ugonjwa wa ebola nchini Tanzania hivyo watanzania msiwe na hofu ila
tuchukue tahadhari na kupata elimu zaidi ili kujikinga na ugonjwa huu”
alisisitiza Waziri Ummy.
Mbali na hayo Waziri Ummy ameamua
kuunda timu huru ya watu sita itakayoongozwa na Daktari Bingwa wa
magonjwa ya kinamama Prof. Charles Majige ili kuchunguza upya tukio la
Bi. Asma Elias ya kuibiwa kichanga katika hospitali ya Temeke baada ya
kukataliwa ripoti ya awali iliyotolewa na Mganga Mkuu wa Dar es salaam.
SHARE
No comments:
Post a Comment