NA HAMZA TEMBA - WMU
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe amemtaka Mkuu wa Mkoa wa
Tabora, Aggrey Mwanry kutumia fursa ya uwepo wa Chuo cha Mafunzo ya
Ufugaji Nyuki, Tabora, BTI mkoani humo kwa kuandaa utaratibu maalum
utakaowawezesha wananchi hususan wafugaji wa nyuki kuhudhuria mafunzo ya
muda mfupi ya ufugaji wa nyuki chuoni hapo kwa ajili ya kuboresha
uzalishaji wa bidhaa hiyo na kuwaongezea kipato.
Waziri
Maghembe ametoa kauli hiyo leo alipotembelea chuoni hapo wakati akiwa
kwenye ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Tabora kwa ajili kujionea
changamoto mbalimbali za uhifadhi na kuona namna kukabiliana nazo ikiwa
ni ahadi aliyoitoa bungeni wakati akihitimisha mjadala wa makadirio ya
mapato na matumizi ya bajeti ya Wizara yake kwa mwaka huu wa fedha
2017/2018.
“Mkuu
wa Mkoa, tafadhali andaa utaratibu maalum kwa wananchi wako, wale
wafugaji wa nyuki wanaweza kuja kwenye chuo chetu hapa hata siku tatu,
hata siku mbili, wafundishwe namna bora ya kufuga nyuki, yani watoke
kabisa huko Skonge, waletwe hapa, walale hapa sku moja au mbili
wafundishwe baadae warudi makwao wajue namna bora ya kufuga na kuvuna
asali,” alisema Maghembe.
Kwa
upande wake Mkuu huyo wa Mkoa wa Tabora alisema maelekezo hayo kwao ni
faraja kwakuwa tayari kuna maelekezo ya kiserikali kusaidia makundi ya
kinamama na vijana ikiwemo utoaji wa mikopo kwa vikundi vyao vya
ujasiriamali.
“Katika
Mkoa wangu tuna makundi haya ya kinamama na vijana ambao tumetakiwa
kuwasaidia kwa maana ya kutenga “percent” (asilimia) fulani katika “own
source” (vyanzo vya ndani vya mapato), kwahiyo kwa maelekezo hayo hayo
nitakachofanya mimi ni kuhakikisha kwamba tunaenda kuwaeleza katika hali
ya kawaida kwamba tungeweza kuwapa mikopo lakini tungependa tuwape
mikopo baada ya kupata taaluma na waweze kujua vizuri namna bora ya
kufuga nyuki na kurina asali”, alisema Mwanri.
Mkuu
wa Chuo hicho, Semu Daudi alisema chuo hicho kina jumla ya wanafunzi
155 na kinatoa mafunzo ya Cheti na Diploma ya Ufugaji wa Nyuki.
Naye
Mkuu wa Kituo kidogo cha Utafiti wa Ufugaji Nyuki chuoni hapo, Humphrey
Natali alisema kituo hicho kinakabiliwa na changamoto ya vitendea kazi
ikiwemo usafiria ambapo gari lililokuwepo limepelekwa matengenezo na
kompyuta zilizopo nazo ni za muda mrefu.
Waziri
Maghembe ameahidi kukipatia kituo hicho gari moja huku akimuagiza,
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Prof. Dos Santos
Silayo kuona uwezekano wa kumaliza changamoto mbalimbali chuoni hapo.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) akizungumza na
uongozi wa chuo cha Mafunzo ya Ufugaji Nyuki, Tabora BTI alipotembelea
chuoni hapo leo. Kulia ni Mkuu wa chuo hicho Semu Daudi na Mratibu Mkuu
wa Mafunzo, Igunda John.
Mkuu
wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanry (kulia) na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa
Huduma za Misitu Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo wakimsikiliza kwa
makini Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe wakati
akitoa maelekezo mbalimbali chuoni hapo.
SHARE
No comments:
Post a Comment