Rais wa Serikali ya Wanafunzi
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (DARUSO) akisisitiza jambo wakati wa
mkutano na waandishi wa Habari uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam
ukilenga kutoa tamko la DARUSO kuhusu kuunga mkono juhudi zinazofanywa
na Serikali hasa matokeo ya Tume ya kuchunguza kiwango cha madini kwenye
makontena 277.Kulia ni Waziri wa Ulinzi wa Serikali hiyo Bw. Richard
Augustine na kushoto ni Waziri Mkuu wa Serikali hiyo Bw. Sintau Fredrick
Rais wa Serikali ya Wanafunzi
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (DARUSO) akisisitiza jambo wakati wa
mkutano na waandishi wa Habari uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam .
(Picha na Frank Mvungi-Maelezo)
…………………
Frank Mvungi-MAELEZO
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amepongezwa na Serikali ya Wanafunzi
wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (DARUSO) kwa kusimamia vyema rasilimali za
Taifa ili ziweze kuwanufaisha watanzania wote.
Kauli hiyo imetolewa leo Jijini
Dar es Salaam na Rais wa (DARUSO) Bw.John Jilili wakati wa mkutano wao
na vyombo vya habari uliolenga kutoa tamko la kuunga mkono juhudi za
Mhe. Rais kwa kuunda Tume iliyochunguza na kutoa matokeo kuhusu mchanga
(makinikia) unaosafirishwa nje ya nchi.
“Kuanzia sasa uchakataji
(processing) ufanyike hapa nchini na mikataba yote iwe na kipengele
kinachoyalazimisha makampuni yanayopewa leseni ya kuchimba madini kuwa
na mitambo ya kuchenjua makinikia ya madini yanayozalishwa na migodi
hiyo.” alisema Jilili
Akifafanua zaidi Jilili amesema
kuwa mikataba yote ya Madini ni vyema ikatazamwa upya na kuzingatia
maslahi mapana ya Taifa na si ya watu wachache, kwani kwa kufanya hivyo
kuonyesha dhamira ya dhati ya Serikali katika kuleta mageuzi katika
sekta ya madini nchini.
Katika mapendekezo yao DARUSO
imebainisha kuwa Watanzania wangependa kuona Mikataba na Sheria zilizopo
zinaruhusu ukaguzi wa mara kwa mara migodini ili Serikali ijiridhishe
kuhusu kiwango cha madini kinachozalishwa katika migodi hiyo pamoja na
Serikali kuwa na ubia wa asilimia 50 au 49 na wawekezaji katika sekta ya
madini.
Aidha Jilili alisema vyema pia kwa
vyema kwa Viongozi wote waliopewa dhamana ya kuwaletea wananchi
maendeleo wakatekeleza wajibu huo kwa uzalendo na kuepuka kuingia
mikataba inayowezesha kuiletea hasara Serikali.
“Tunapenda kuwaomba watanzania
wote wasomi na wasio wasomi kumsaidia Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli
kufikia lengo lake la kuleta mageuzi makubwa ya kiuchumi na hayo
yanawezekana tu kwa kuweka uzalendo mbele na maslahi ya Taifa kwanza.”
Alisisitiza Jilili
Aliongeza kuwa nidhamu na
uwajibikaji katika sehemu za kazi ni jambo la muhimu kwa Watendaji
waliokabidhiwa majukumu ya kusimamia sekta mbalimbali kwani kwa kufanya
hivyo kutawezesha kuzaliwa kwa Tanzania mpya chini ya Uongozi wa
Serikali ya awamu ya Tano.
“DARUSO inamthibitishia Mhe. Rais
Dkt. John Pombe Magufuli na Watanzania wote kuwa iko sambamba nae katika
harakati zake za kuikomboa nchi yetu katika Nyanja zote ikemo kiuchumi”
Alisisitiza Jilili
SHARE
No comments:
Post a Comment