TRA

TRA

Wednesday, May 3, 2017

Siku ya Uhuru wa Habari Duniani

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !

Dunia leo inaadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya habari, na Shirika la Utangazaji la Ujerumani Deutsche Welle limesema litatoa tuzo ya kila mwaka ya uhuru wa kujieleza kwa Chama cha Wanahabari wa Masuala ya Ikulu ya White House, kutokana na mchango wao wa "kuhakikisha uwajibikaji wa uongozi wa Marekani". 

DW imesema leo kuwa rais wa chama hicho cha wanahabari wa Ikulu ya White House Jeff Mason atakabidhiwa tuzo hiyo mjini Bonn, hapa Ujerumani mnamo Juni 19. 


Sansibar Kiosk mit Zeitungen (picture-alliance/dpa/A. Gebert) Wananchi wakiangalia vichwa vya habari vya magazeti Tanzania

Washindi wa awali wa tuzo hiyo, iliyozinduliwa miaka miwili iliyopita, ni mwnaablogu wa Saudia anayeizuiliwa Raif Badawi na Sedat Ergin, wakati huo akiwa Mhariri Mkuu wa gazeti la Uturuki la Hurriyet. 

DW imesema licha ya rais wa sasa wa Marekani kuwanyima uaminifu wao na wakati mwingine uadilifu wao kushambiliwa, wanahabari hao wameweka kiwango chao juu katika kuripoti kuhusu sera za utawala mpya wa Marekani.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger