Mahakama ya juu ya Urusi imepitisha uamuzi unaopiga marufuku
madhehebu ya Mashahidi wa Yehova nchini humo.
Uamuzi huo umeamuru kufungwa kwa makao makuu ya madhehebu hayo na matawi yake yapatayo 395.
Mashahidi wa Yehova vile vile wameamuliwa kukabidhi mali ya madhehebu yao kwa taifa la Urusi.
Rais wa Urusi, Vladmir Putin
Hatua hiyo ya mahakama ya juu ya Urusi imefuatia uamuzi wa wizara ya sheria ya nchi hiyo, ambayo ilisema imebaini shughuli zinazoashiria misimamo ya kupindukia katika madhehebu hayo, na kutaka yapigwe marufuku.
Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limesema hatua hiyo ni kikwazo cha uhuru wa kuabudu nchini Urusi.

No comments:
Post a Comment