Baraza la uangalizi nchini Iran limemzuia rais wa zamani wa nchi hiyo
Mahmoud Ahmadinejad kuwa mgombea katika uchaguzi wa rais utakaofanyika
mwezi ujao.
Ahmadinejad mwenye misimamo mikali aliwashtusha wairan wiki
iliyopita, alipotangaza nia yake ya kuingia tena katika kinyang'anyiro
cha urais.
Mahmoud Ahmadinejad
Kituo cha televisheni ya taifa ya Iran kimesema baraza lenye
jukumu la kuchunguza majina ya wagombea, limeliondoa jina lake katika
orodha ya watakaowania wadhifa huo.
Rais wa sasa Hassan Rouhani ni mmoja
wa wagombea sita ambao wameridhiwa na baraza hilo.
No comments:
Post a Comment