Mtendaji Mkuu wa TAHA, Jacqueline Mkindi
(kulia) akimkaribisha Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania
(TADB), Francis Assenga (kushoto) wakati wawili hao walipokutana kujadiliana
juu ya kushirikiana katika kuisaidia sekta ya malimbichi na matunda nchini.
Mkutano huo ulifanyika Makao Makuu ya TAHA, Jijini Arusha.
Timu
ya Maandalizi ya Makubaliano ya ushirikiano katika kuisaidia sekta ya
malimbichi na matunda nchini wakiwa katika majadiliano.
Mtendaji Mkuu wa TAHA, Jacqueline Mkindi
(kushoto) akihimiza jambo juu ya umuhimu wa sekta ya malimbichi na matunda
katika uchumi wa Tanzania kwa Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo
Tanzania (TADB), Francis Assenga (hayupo pichani) wakati wawili hao
walipokutana kujadiliana juu ya kushirikiana katika kuisaidia sekta ya
malimbichi na matunda nchini. Mkutano huo ulifanyika Makao Makuu ya TAHA,
Jijini Arusha. Kulia ni Meneja Mkuu wa Maendeleo wa TAHA, Anthony Chamanga.
Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB),
Francis Assenga (kulia) akimuelezea Mtendaji Mkuu wa TAHA, Jacqueline Mkindi
(hayupo pichani) nafasi ya TADB katika kuleta mapinduzi ya kilimo
nchini. Kushoto ni Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara, Augustino Chacha
Mtendaji Mkuu wa TAHA, Jacqueline Mkindi
akieleza utayari wa TAHA wa kushirikiana na TADB katika kukwamua changamoto
zinazoikabili sekta ya malimbichi na matunda nchini.
Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya
Kilimo Tanzania (TADB), Francis Assenga (kushoto) akizungumza na Mtendaji Mkuu
wa TAHA, Jacqueline Mkindi (kulia) nafasi ya TADB katika kuchagiza na kusaidia
Mapinduzi ya Kilimo kutoka kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara
ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini. Mkutano huo
ulifanyika Makao Makuu ya TAHA, Jijini Arusha.
Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya
Kilimo Tanzania (TADB), Francis Assenga (kushoto) akizungumza na Mtendaji Mkuu
wa TAHA, Jacqueline Mkindi (kulia) mara baada ya mkutano wao unaolenga
kuisaidia sekta ya malimbichi na matunda nchini. Mkutano huo ulifanyika Makao
Makuu ya TAHA, Jijini Arusha
BENKI ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania
(TADB) na Asasi Kilele ya wakulima wa Malimbichi na Matunda Tanzania (TAHA)
zinajipanga kusaidia sekta Malimbichi na Matunda (horticulture) ili kuongeza
tija kwa kilimo hicho.
Watendaji wakuu wa taasisi hizo wamesema
kuwa kuna haja ya makusudi ya uwekezaji mkubwa katika sekta ya Malimbichi na
Matunda (horticulture) ili kuchagiza na kusaidia mapinduzi katika sekta hiyo na
kilimo kwa ujumla nchini.
“Tunajipanga kuchochea ukuaji wa sekta hii
ili kuwakwamua wakulima wa malimbichi kutoka kilimo cha
kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na
kupunguza umaskini nchini,” anasema Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa
TAHA, Jacqueline Mkindi amesema kuwa kuna umuhimu mkubwa wa ushirikiano kati ya
TADB na TAHA kwa kuwa taasisi zote ni za Kilele (apex institutions) zenye
kulenga katika kuleta mapinduzi ya kilimo Tanzania kutoka kilimo cha kujikimu
kwenda katika kilimo cha kibiashara na uzalishaji wenye tija katika kukuza
uchumi na kupunguza umaskini.
SHARE
No comments:
Post a Comment