Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe.
Joel Bendera (katikati) akimkaribisha Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB,
Bw. Francis Assenga (kushoto) wakati alipomtembelea ofisini kwake.
Kulia ni Mrajis Msaidizi wa Mkoa wa Manyara, Bw. Venance Msafiri.
Mrajis Msaidizi wa Mkoa wa
Manyara, Bw. Venance Msafiri (kulia) akimtambulisha Kaimu Mkurugenzi
Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (kushoto) kwa Mkuu wa Mkoa wa
Manyara, Mhe. Joel Bendera (katikati).
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa
TADB, Bw. Francis Assenga (kushoto) akitambulisha mikopo na huduma
zinazotolewa na Benki yake kwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe. Joel
Bendera (kulia).
Mrajis Msaidizi wa Mkoa wa
Manyara, Bw. Venance Msafiri (kulia) akizungumzia hali ya ushirika
mkoani Manyara wakati wa ugeni wa TADB walipotembelea Ofisi ya Mkuu wa
Mkoa wa Manyara. Wanaomsikiliza ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe. Joel
Bendera (katikati) na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis
Assenga (kushoto).
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe.
Joel Bendera (katikati) akizungumzia fursa za uwekezaji katika kilimo na
mifugo zinazopatikana mkoani Manyara wakati Kaimu Mkurugenzi Mtendaji
wa TADB, Bw. Francis Assenga (kushoto) alipomtembelea ofisini kwake.
Kulia ni Mrajis Msaidizi wa Mkoa wa Manyara, Bw. Venance Msafiri.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe. Joel Bendera akisisitiza umuhimu wa TADB kwa mkoa wa Manyara.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa
TADB, Bw. Francis Assenga (kushoto) akimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa
wa Manyara, Mhe. Joel Bendera wakati akisisitiza umuhimu wa TADB
kuwekeza mkoani Manyara.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga akisisitiza utayari wa Benki yake kuwekeza mkoani Manyara.
…………………………………………………………………….
Na mwandishi wetu, Manyara
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe.
Joel Bendera ameiomba Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB)
kwenda kuwekeza mkoani humo kwa kuwapatia kuwapatia mikopo na mahitaji
mengine kwa ajili ya kuongeza tija kwa wakulima wa mkoa huo.
Akizungumza wakati wa mazungumzo
na ugeni kutoka TADB uliomtembelea Ofisini kwake, Mhe. Bendera amesema
mkoa wa Manyara una fursa nyingi za uwekezaji katika sekta ya kilimo na
mifugo kulinganisha na mikoa mingini nchini.
“Mkoa wa Manyara una fursa nyingi
sana ambazo Benki inaweza kutoa mikopo ambayo nina uhakika itarudishwa
kwa wakati kwa sababu watu wa Manyara ni waaminifu sana,” alisema Mhe.
Bendera.
Akizungumza na Mhe. Bendera,
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga amesema Serikali
iliamua kuanzisha Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) ili
kusaidia kukabiliana na mapungufu ya wakulima nchini kote ili kuhuisha
upatikanaji wa mikopo katika sekta ya kilimo na kuchagiza mapinduzi
katika kilimo nchini.
Bw. Assenga ameongeza kuwa sekta
za kilimo na mifugo ni sekta za kipaumbele ambazo zinazopatiwa mikopo
kwa ajili ya uongezaji wa thamani mazao na mifugo mbalimbali hasa katika
uongezaji wa thamani wa sekta hizo nchini.
Ameongeza kuwa Benki yake imejipanga kuendeleza uongezaji wa thamani wa sekta hizo ili kuongeza tija sekta hizo.
“Benki inatoa mikopo ya aina tatu
ambayo ni Mikopo ya Muda Mfupi (Hadi Miaka Miwili (2)), Mikopo ya Muda
wa Kati (Zaidi ya Miaka 2 hadi Miaka Mitano (5)) na Mikopo ya Muda Mrefu
(Zaidi ya Miaka 5 hadi Miaka Kumi na Mitano (15)).
“Mikopo hii ni ya riba nafuu
ambayo inalenga katika kuchagiza na kusaidia Mapinduzi ya Kilimo
kutoka kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye
ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini,” aliongeza.
TADB ni taasisi ya serikali
ambayo ilianzishwa kwa ajili ya kutatua ufinyu mkubwa wa upatikanaji wa
fedha mikopo kwa ajili ya maendeleo ya kilimo nchini ambao ulikuwa
unachangiwa kwa kiasi kikubwa na mikopo mingi kutoka taasisi za fedha
kuelekezwa zaidi kwenye upande wa biashara za bidhaa; riba kubwa kwenye
mikopo ya kilimo; mikopo ya muda mfupi; masharti magumu ya kukopa bila
kuzingatia hali halisi ya sekta ya kilimo na mazao ambayo inaathiriwa
kwa kiasi kikubwa na mabadiliko ya hali ya hewa.
SHARE
No comments:
Post a Comment