NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said
SHIRIKA
la Umeme Tanzania, (TANESCO), limewaomba wateja wake na wananchi kwa ujumla
kutoa taarifa mapema mara inapotokea hitilafu ya umeme iliyosababishwa na mvua
au sababu nyingine.
Akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo Mei 11, 2017,
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka, (pichani juu), alisema, sambamba na
hilo pia wananchi wasifanye shughuli au kukaa chini ya miundombinu ya umeme.
“Lakini
tunawaomba wananchi watoe taarifa haraka maeneo yenye mafuriko au mkusasnyiko
wa maji mengi ili wataalamu wetu waweze kuchukua hatua za haraka.” Alisema.
Dkt.
Mwinuka pia alisema endapo kuna nyaya, nguzo au kifaa chochote cha umeme
kimepata hitilafu na kinahatarisha maisha ni vema uangalizi au alama ikawekwa
ili kuwapa hadhari wapiti njia na watoto wasikaribie eneo hilo wakati mafundi wa
TANESCO wakichukua hatua za marekebisho.
Mamlaka
ya Hali ya Hewa nchini Tanzania (TMA), katika taarifa yake iliyotoa Mei
9, 2017
imeonya kuwa maeneo ya Pwani ya Kaskazini ikiwemo visiwa vya Unguja na
Pemba,
yatakabiliwa na vipindi vifupi vya mvua kubwa inayozidi milimita 50
ndani ya
saa 24 kuanzia Mei 10 hadi 12, 2017. Aidha kwa upande wake, mtaalamu wa
masualaya umeme kutoka TANESCO, Mhandisi Simon Kihiyo, amewahakikishia
wananchi kuwa miundombinu ya TANESCO iko imara na salama, na hitilafu
zinazotokea za hapa na pale nyingizinasababishwa na sababu za
kibinadamu, au za kimazingira kama vile nguzo za umeme kugongwa na
magari, au miti kuangukia nguzo. "Naomba nitoe angalizo kwa wateja wetu,
kama pametokea hitilafu yoyote ya umeem nyumbani kwako, ni vema ukatoa
taarifa TANESCO au ukamtafuta fundi wa umeme mwenye taaluma badala ya
kushughulikia tatizo hilo wewe mwenyewe ilihali ukiwa huna utaalamu na
masuala ya umeme, kwani hiyo ni hatari."
Naye
kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO Leila Muhaji amesema, katika kipindi
hiki cha mvua kuna athari ndogo ndogo zimetokea kwenye miundombinu ya
TANESCO hususan nguzo za umeme, lakini akatoa hakikisho kuwa mafundi wa
TANESCO wanekuwa wakichukua hatua za haraka kurekebisha athari katika
miundombinu ya umeme pindi tu zinapotokea.
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Dkt. Tito Mwinuka,
(katikati), akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es
Salaam, Me11, 2017. Dkt. Mwinuka ametoa hadhari kwa wananchi kutogusan
miundombinu ya Tanesco hususan nyaya zilizoanguka, au kufanya shughuli yoyote
karibu na miundombinu yab umeme katika kipindi hiki cha mvua kubwa zinazoendela
kunyesha nchini. Kulia ni Mhandisi Simon Kihiyo, na kushoto ni Kaimu Meneja
Uhusiano wa TANESCO, Leila Muhaji.
Mhandisi Simon Kihiyo, akitoa ufafanuzi wa kitaalamu kuhusu hatua za kuchukua pindi hitilafu ya umeme inapotokea
Dkt. Mwinuka (kushoto) na MhandisiKihiyo, wakati wa mkutano huo leo
Dkt. Mwinuka akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake
Waandishi wa habari wakiwa kazini
Waandishi wa habari wakiwa kazini
Kaimu
Meneja
Uhusiano wa TANESCO, Leila Muhaji, akitoaufafanuzi zaidi wa hatua za
kuchukua endapo wateja au wananchi wataona hitlafu ya umeme kwenye
maeneo yanayowazunguka
Mhandisi Kihiyo, (kulia0na Kaimu Meneja Uhusianowa TANESCO Leila Muhaji katika mkutano na wanahabari
Mhandisi Simon Kihiyo, (kulia), Kaimu
Meneja Uhusiano wa TANESCO, Leila Muhaji (kushoto) na Afisa Uhsiano wa
Shirika hilo, Henry Kilasila wakijadiliana jambo.
SHARE
No comments:
Post a Comment