Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa
Shinyanga,Mheshimia Azza Hilal Hamad kupitia tiketi ya Chama Cha
Mapinduzi (CCM)ametembelea Zahanati ya Solwa iliyopo katika kijiji cha
Solwa,kata ya Solwa,jimbo la Solwa mkoa wa Shinyanga kisha kutoa msaada
wa viti vya kisasa vya kujifungulia kwa akina mama,vifaa vinavyotumika
katika chumba cha kujifungulia na viti vya wagonjwa (wheel chairs) vyote
vikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni nne.
Vifaa hivyo ni miongoni mwa vifaa tiba alivyovipata kutoka Ubalozi wa China nchini Tanzania kwa lengo la kupunguza vifo vya mama na mtoto katika zahanati,vituo vya afya na hospitali mkoani Shinyanga.
Akitoa msaada huo leo Alhamis May 11,2017 Mheshimiwa Azza Hilal Hamad alisema msaada huo utasaidia katika kupunguza vifo vinavyotokana na uzazi kwa kuwarahishia akina mama kupata huduma karibu badala ya kutembea umbali kufuata huduma za afya.
“Mimi ni mama nazifahamu changamoto wanazokabiliana nazo akina mama,nilitafakari na kuangalia nani wa kuweza kutusaidia,nikaenda ubalozi wa China nchini kuomba wasaidie akina mama wa Shinyanga,walikubali na leo nimeleta vitanda vya kisasa kwa ajili ya akina mama,viti vya wagonjwa na vifaa vinavyotumika katika chumba cha kujifungulia”,alieleza Hamad.
Katika hatua nyingine mbunge huyo
aliwapongeza wananchi wa Solwa kwa kujitolea na kuanza ujenzi wa jengo
la wodi ya akina mama katika zahanati ya Solwa ambapo ameahidi kuwapatia
mabati 20 kwa ajili ya paa la jengo hilo.
Aidha aliwataka wananchi kuachana na
tabia ya kuwaozesha watoto wa kike na badala yake wawatafutie shughuli
zingine za kufanya wanapofeli mtihani wa darasa la saba kwani wakiolewa
wangali wadogo husababisha wapoteze maisha wakati wa kujifungua hivyo
kuchangia ongezeko la vifo vya mama na mtoto katika jamii.
Mheshimiwa Hamad pia aliahidi kutafuta
namna ya kumsaidia mtoto Salawa Mihangwa (03) ambaye ana tatizo la
ugonjwa wa moyo na amekuwa akilelewa na kupatiwa huduma za kiafya katika
zahanati hiyo baada ya mzazi wake Grace Richard kukosa shilingi milioni
2.6 kwa ajili ya mtoto huyo kufanyiwa upasuaji katika hospitali ya
taifa ya Muhimbili.
Mwandishi wetu Kadama Malunde,alikuwepo katika zahanati ya Solwa,ametuletea picha 25 za matukio yaliyojiri,Tazama hapa chini
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga
Azza Hilal Hamad, (CCM) akizungumza na wananchi wa kijiji cha Solwa kata
ya Solwa jimbo la Solwa mkoani Shinyanga alipotembelea zahanati ya
Solwa kisha kukabidhi msaada wa viti viwili vya kisasa vya kujifungulia
kwa akina mama,viti viwili kwa ajili ya wagonjwa na vifaa vinavyotumika
katika chumba cha kujifungulia kwa akina mama
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa
Shinyanga,mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akizungumza wakati wa
kukabidhi vifaa tiba vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni nne
katika zahanati ya Solwa
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga
Azza Hilal Hamad (CCM) akizungumza wakati wa kumkabidhi Mganga Mfawidhi
wa zahanati ya Solwa Dkt. Edwin Ibrahim (kulia) vifaa vinavyotumika
katika chumba cha kujifungulia akina mama (alivyoshikilia Dkt. Ibrahim )
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga
Azza Hilal Hamad (CCM) akishikana mkono na mwenyekiti wa kijiji cha
Solwa Emmanuel Ngamba wakati akikabidhivitanda vya kujifungulia,viti vya
wagonjwa na vifaa vinavyotumika kwenye chumba cha kujifungulia akina
mama
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga
Azza Hilal Hamad (CCM) akionesha baadhi ya vifaa vinavyotumika katika
chumba cha kujifungulia
Kushoto ni Mwenyekiti wa UWT wilaya ya
Shinyanga Hellena Daudi akiwa na baadhi ya madiwani wa CCM wakati wa
zoezi la kukabidhi vifaa tiba katika zahanati ya Solwa
Katibu wa UWT mkoa wa Shinyanga Angel Robert akizungumza wakati wa makabidhiano ya vifaa tiba katika zahanati ya Solwa
Diwani wa kata ya Solwa Shadrack Awadh akielezea matatizo yanayokabili wananchi wa kata hiyo
Wazee wa kata ya Solwa wakikabidhi zawadi ya mbuzi kwa mbunge Azza Hilal Hamad
Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akiteta jambo na mmoja wa wazee wanaoishi katika kata ya Solwa
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa
Shinyanga,mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akiwa amebeba mtoto katika
chumba kinachotumika kama wodi ya akina mama katika zahanati ya Solwa
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa
Shinyanga,mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akishiriki ujenzi wa jengo
la wodi ya akina mama katika zahanati ya Solwa ambapo aliahidi kutoa
mabati 20 kusaidia ujenzi huo ambao umetokana na nguvu za wananchi
walioamua kuchangishana pesa na kuanza kujenga ili kukabiliana na
changamoto ya vifo vya akina mama na watoto
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa
Shinyanga,mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akishiriki ujenzi wa jengo
la wodi ya akina mama katika zahanati ya Solwa
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa
Shinyanga,mheshimiwa Azza Hilal Hamad akiweka tofali wakati akishiriki
ujenzi wa jengo la wodi ya akina mama zahanati ya Solwa
Wa pili kutoka kushoto ni mganga
mfawidhi katika zahanati ya Solwa, Dkt. Edwin Ibrahim akielezea kuhusu
mradi wa Lishe wanaoutoa katika zahanati hiyo kukabiliana na tatizo la
utapiamlo kwa watoto lililokithiri katika jimbo la Solwa. Dkt. Ibrahim
alimweleza mbunge Azza Hilal Hamad kuwa zahanati hiyo imekuwa ikitoa
elimu ya lishe kwa akina mama na kutoa chakula dawa kwa ajili ya watoto
ambao hali zao kiafya siyo nzuri (wenye utapiamlo)
Ndani ya chumba cha lishe-Mheshimiwa
Azza Hilal Hamad na diwani wa kata ya Solwa Shadrack Awadh wakiangalia
chakula dawa ( unga maalum wenye lishe) 'Multiple Micronutrient powder)
kinachotolewa kwa watoto wenye utapiamlo wanaofika katika zahanati ya
Solwa
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa
Shinyanga,mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akiwa amembeba mtoto Salawa
Mihangwa (03) ambaye ana tatizo la ugonjwa wa moyo na amekuwa akilelewa
katika zahanati ya Solwa baada ya mzazi wake Grace Richard (kushoto)
kukosa shilingi milioni 2.6 kwa ajili ya mtoto huyo kufanyiwa upasuaji
katika hospitali ya taifa ya Muhimbili.
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa
Shinyanga,mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akimweleza mama wa mtoto
huyo kuwa ameguswa na hali ya mtoto huyo ambaye afya yake siyo nzuri
hivyo kuahidi kutumia mbinu mbalimbali ili mtoto aweze kufanyiwa huduma
ya upasuaji
Mganga Mfawidhi wa zahanati ya Solwa
Dkt. Edwin Ibrahim akimwonesha mheshimiwa Azza Hilal Hamad vyeti vya
mtoto Salawa Mihangwa anayesumbuliwa na ugonjwa wa moyo na amekuwa
akilelewa katika zahanati ya Solwa ambayo sasa inalea watoto 95 wenye
tatizo la utapiamlo huku mtoto anayesumbuliwa na ugonjwa wa moyo akiwa
mtoto wa kwanza kulelewa katika zahanati hiyo
Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akizungumza
na akina mama wenye watoto wanaolelewa katika zahanati ya Solwa kutokana
na watoto kukabiliwa na utapiamlo ambapo aliwasisitiza kuwapatia watoto
mlo kamili na kuzingatia ushauri wanaopewa na wataalam wa masuala ya
afya
Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akigawa matunda kwa watoto wanaopata huduma ya lishe katika zahanati ya Solwa
Mganga Mfawidhi wa zahanati ya Solwa
Dkt. Edwin Ibrahim akimwonesha mheshimiwa Azza Hilal Hamad shamba la
viazi lishe vilivyolimwa katika zahanati ya Solwa kwa ajili ya watoto
wanaohudumiwa katika zahanati hiyo kukabiliana na tatizo la utapiamlo
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga
Azza Hilal Hamad kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) akiondoka
katika zahanati ya Solwa baada ya kukabidhi vifaa tiba vitakavyosaidia
kupunguza vifo vya akina mama na watoto.
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
SHARE
No comments:
Post a Comment