TRA

TRA

Monday, May 15, 2017

TANI 16 ZA SUKARI ZA KUTWA KWENYE GHALA LA AFISA MIPANGO KIMAGENDO

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !

Baadhi ya Sukari iliyokamatwa  ikiwa inabadilihwa kutoka mifuko ya Tanzania na kuwekwa katika mifuko ya Nchi jirani ya Kenya.




Jengo la Forodha mpaka wa Sirari

Meneja TRA Mkoa wa Mara Erenest Nkangaza akiangalia mifuko ya Kenya ambayo inatumika kuwekewa sukari ya Tanzania.



Mifuko ya Sukari kutoka Nchi jirani ya Kenya iliyokuwa ikipakiwa Sukari ya Tanzania ili kupelekwa Kenya.

Tani 16 za sukari ya Magendo zimekutwa na jeshi la polisi kwenye ghala la afisa Mipango wa manispaa ya Musoma John Masero katika kijiji cha Nyabisaga kata ya Pemba Wilayani hapa mkoani Mara.

Kaimu kamanda wa mkoa wa polisi Tarime/Rorya Sweetbert Njewike alisema watu 20 akiwepo afisa mipango wa manisapaa ya Musoma wanashikiliwa na jeshi hilo baada ya kukutwa wakifanya kazi ya kubadilisha sukari kutoka kwenye mifuko yenye nembo ya kiwanda cha sukari cha Kagera kwenda kwenye mifuko yenye nembo ya kampuni ya Sonny Sugar ya Nchini Kenya.

Meneja  wa mamlaka ya  mapato mkoani Mara (TRA) Erenest Nkangaza alisema kuwa watu hao walikuwa katika harakati za kubadilisha sukari ya tanzanikutoka kwenye mifuko yake na kuika kwenye mifuko ya kiwanda cha Sukari cha Sonny cha nchini Kenya.

“wakati serikali ikiwa kwenye upungufu mkubwa wa sukari ndipo watanzania wanafanya kuhujumu sukari ya viwanda vyetu kupeleka Kenya ili kukwepa kodi, hili tunalifanyia kazi na tayari tunawashirikilia watu 20 akiwemo mmiliki wa ghala hilo ambao baada ya uchunguzi kukamilika sheria itafuata mkondo wake,”alisema Nkangaza.

Aliongeza kuwa mafanikio hayo yametokana na uchunguzi mzuri wa vyombo vya ulinzi uliofanyika katika eneo hilo na kufanikiwa kutambua ghala hilo ambalo limekuwa likitumika kufanya uhujumu huo kwa kukwepa kodi ili kujipatia faida nyingi.

“Baada ya kufika katika ghala hilo tulifikili kuwa ni sukari ya kagera tu lakini kumbe kulikuwa na mifuko ya TPC na Kilombero huu ni ushahidi tosha kuwa watu hawa wamekuwa wakifanya hivi kwa muda mrefu na wajue kuwa biashara ya magendo haikubaliki, utaratibu ni mzuri tu kupitisha bidhaa kwenye mpaka wetu wa sirari tunatoa huduma nzuri tunawaomba wafanyabiashara waache,” alisema Nkangaza.

Kutokana na hali ya wafanya biashara kutorosha shehena za bidhaa hasa sukari bei ya bidhaa hiyo imepanda kutoka sh, 2600 kwa mwezi wa tatu hadi sh, 3600 kwa kila huku mfuko wa kilogramu 25 ikiizwa kwa sh, 70,000 na 140,000 -145000 kwa mfuko wa kilogramu 50 katika mpaka wa Sirari.

Aidha katika uchunguzi uliofanyika na vyombo vya ulinzi umeonyesha kuwa zoezi la kubadilisha sukari kutoka kwenye mifuko ya Viwanda vya serikali ya Tanzania kwenda kwenye viwanda vya nchi jirani ya Kenya.

“Ushahidi unaonyesha kubwa kiasi kikubwa kimekuwa kikitoroshwa kutokana na mazingira ambayo tumeyaona katika hilo ghala jambo ambalo linazuia wananchi kupata bidhaa hii kwa urahisi,”alisema Nkangaza.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Tarime Glorious Luoga amesema kuwa Serikali imejipanga vyema kwa lengo la kutokomeza suala zima la magendo ili kuweza kukusanya mapato.

“Wafanyabiashara wafuate taratibu zote katika mpaka wa sirari na siyo kufanya biashara ya Magendo” alisema Louga.






Meneja TRA Mkoa wa Mara Erenest Nkangaza akiongea na Vyomba vya habari

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger