Ofisa wa Mtandao wa Kijinsia
Tanzania (TGNP), Veronica Magayane akitoa mada wakati wa mkutano wa
uchambuzi wa bajeti ya wizara hiyo kwa mlengo wa kijinsia uliofanyika
jijini Dar es Salaam jana.
Wadau wakiwa kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Uchambuzi wa bajeti hiyo ukiendelea.
Mzee Hamisi Katumwa akichangia jambo kwenye mkutano huo.
Mdau Msafiri Mtakatifu akichangia jambo.
Mdau Wilfred akichangia jambo kuhusu bajeti hiyo.
Bi. Ester Tibaigana akichangia jambo.
Muonekano wa chumba cha mkutano huo wakati wa uchambuzi wa bajeti hiyo.
Bi. Marytaus Mbawala akichangia mada.
Na Dotto Mwaibale
MTANDAO
wa Jinsia Tanzania (TGNP) umesema bajeti ya mwaka 2017/2018 ya Wizara
ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi iliyopitishwa na bunge haijatoa
kipaumbele kwa mtoto wa kike.
Hayo
yalibainishwa na Ofisa wa TGNP, Veronica Magayane wakati akitoa mada
katika mkutano wa uchambuzi wa bajeti ya wizara hiyo kwa mlengo wa
kijinsia uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Alisema
licha ya bajeti hiyo kupitishwa na bunge haijaangalia changamoto
zinazomkabili mtoto wa kike kama umbali kutoka makazi na shule, kiwango
cha walimu kisicholizisha, kutokuwepo kwa mabweni ya watoto wa kike,
kufanyishwa kazi nyumbani kwa walimu kama kuchota maji na kuwapakia
walimu.
Alitaja
changamoto zingine ni kukosekana kwa maji ambapo kumechangia kuwafanya
watoto hao wa kike kuwa katika wakati mgumu hasa wanapokuwa kwenye
hedhi.
“Changamoto hizi zote zimesababisha elimu kwa mtoto wa kike kushuka na kupelekea wengi wao kutofikia ndoto zao” alisema Magayane
Alisema
matatizo mengi ya miundombinu ambayo huathiri zaidi watoto wa kike
yanatokana na changamoto za mfumo wa bajeti ya sekta ya elimu hivyo
suala la kuboresha miundombinu ya shule linapaswa kuwa kipaumbele zaidi
kwa kuongeza fedha za bajeti ya maendeleo.
Akichangia katika mjadala huo, Mzee Hamisi Katumwa alisema kuna kila sababu ya kutenganisha Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi)
na Wizara ya Elimu ili kupunguza kutupiana mpira ambapo kumekuwa na
ucheleweshaji wa maamuzi ambapo mtu akienda Tamisemi anaambiwa suala
hilo ni la wizara na akienda wizarani anaambiwa ni la Tamisemi.
Msafiri
Mtakatifu alisema kwa wakati huu kipaumbele kinachopaswa kutiliwa mkazo
zi barabara za juu wala ununuzi wa ndege bali ni elimu kwanza mambo
mengine yafuate baadae.
Gilbert
Nelson alisema ili kuinua elimu inatakiwa wizara hiyo kutengewa bajeti
ya kutosha na kuwepo na uwekezaji mkubwa kama serikali inavyofanya
katika maeneo mengine.
“Hatuwezi kuingia katika uchumi wa maendeleo ya viwanda bila ya kuwa na watu wenye elimu” alisema Nelson.
Mwaka
2016/2017 katika bajeti ya Wizara ya Elimu iliidhinishwa shilingi
bilioni 277 sawa na asilimia 31 ilikadiriwa kukusanywa kutoka kwa
wahisani na washirika wa maendeleo.
Katika mwaka huu wa fedha wa
2017/2018 serikali imekadiria kukusanya kutoka kwa wahisani na washirika
wa maendeleo shilingi bilioni 310 sawa na asilimia 33.7 ya fedha ya
maendeleo ikiwa ni ongezeko la utegemezi kwa asilimia 10.6.(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)
SHARE
No comments:
Post a Comment