Jeshi la Polisi nchini linapenda
kutoa ufafanuzi kuwa, Fomu ya Polisi namba 3 ijulikanayo kama PF.3
hutolewa kwa mtu baada ya Polisi kupata taarifa kutoka kwa mlalamikaji
au muathirika kwa matukio yenye madhara mwilini, ajali au matukio
yenye kuleta mashaka kuhusu vyanzo vyake kama vile kipigo, kujeruhi,
ubakaji, kulawiti, kunywa sumu na mengineyo.
Ieleweke wazi kwamba matumizi ya
PF3 ni ya lazima na yanaendelea kama kawaida kwa mujibu wa sheria, fomu
hiyo inapaswa kutumika kwa kila tukio la aina tajwa hapo juu ili
muathirika aweze kupata matibabu katika vituo vya Afya na hatua za
kiupelelezi kwa Jeshi la Polisi ziweze kuendelea.
Katika mazingira mengine hali ya
muathirika inaweza kuwa mbaya, hivyo, huduma za kuokoa maisha (huduma
ya kwanza) zinaweza kuendelea kutolewa wakati watoa huduma ya afya
wakiijulisha Polisi ili kuharakisha upatikanaji wa PF 3.
Imetolewa na:-
Advera Bulimba-ACP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Makao Makuu ya Polisi.
SHARE
No comments:
Post a Comment