WATU waliopembezoni ambao wamekuwa na shida kubwa ya kupata
madaktari bingwa, wataanza kupata nafuu baada ya kuanza kwa mradi wa
tiba mtandao unaoendeshwa kwa pamoja kati ya Chuo Kikuu cha Afya na
Sayansi-Muhimbili, UNESCO pamoja na wadau wengine. Hayo yalisemwa katika warsha ya siku mbili ya kujadili na kuiangalia dhana ya tiba mtandao na namna ya kuitekeleza. Kwa mujibu wa Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi,
Elimu na Utamaduni (UNESCO) Zulmira Rodrigues utoaji huo wa tiba mtandao
kwa majaribio utaanza mapema zaidi kabla ya mwezi Oktoba mwaka huu. Mratibu
wa E-Medicine kutoka Idara ya Tiba Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto, Dr. Liggy Vumilia akisoma hotuba kwa niaba ya
Katibu Mkuu wa wizara hiyo wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku mbili ya
kujadili na kuiangalia dhana ya tiba mtandao na namna ya kuitekeleza
inayoendelea katika ukumbi wa MUHAS jijini Dar Es Salaam.Alikuwa anatarajia mifumo yote kuwa tayari ifikapo Julai na hivyo
kuwa na nafasi ya kuwa katika matibabu ifikapo Oktoba. Katika warsha
hiyo aliwahimiza wataalamu kujadiliana kiundani changamoto mbalimbali na
namna ya kuweka ripoti ili kuja kusaidia wakati mradi utakapoenda
kitaifa. Katika warsha hiyo iliyokutanisha wataalamu mbalimbali wa tehama na
madaktari kutoka Arusha, Manyara, Kilimanjaro na Dar es Salaam Katibu
Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk
Mpoki Ulisubisya katika hotuba yake ya ufunguzi iliyosomwa na Dk Liggyle
Vumilia alielezea matumaini yake kuhusiana na mradi huo wa majaribio. Aliwataka washiriki wa warsha hiyo kuona uwezekano wa kuanza mradio
huo mapema zaidi baada ya kuhakikisha kwamba dhana imekubalika na namna
ya kuitekeleza inaeleweka miongoni mwa wadau. Naibu
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi-Muhimbili (MUHAS), Prof
Eligius Lyamuya alipokuwa akitoa neno la ukaribisho kwa washiriki wa
warsha ya siku mbili ya kujadili na kuiangalia dhana ya tiba mtandao na
namna ya kuitekeleza inayoendelea chuoni hapo jijini Dar es Salaam.Mradio huo unaoanza kwa majaribio kufuatia juhudi za UNESCO
zilizoanzishwa kwa msaada wa Samsung unahusisha zaidi wagonjwa wanaoweza
kufika kupata matibabu katika kijiji cha kidigitali cha Ololosokwan na
kwa kuanzia huduma hiyo itatolewa kwa mama na mtoto na afya ya kinywa,
masikio, pua na koo (ENT), ambapo mabingwa kutoka KCMC na MUHAS wanaweza
kufanya tiba kwa kutumia mtandao. Kliniki ya Digitali ilizinduliwa katika kijiji cha Ololosokwan Ngorororo, Arusha mnamo mwezi Novemba mwaka 2016. Wataalamu hao kutoka Shirika la Afya Duniani, Mwakilishi wa Tamisemi,
Wizara ya Afya, DMO wa Ngorongoro, wataalamu kutoka KCMC na MUHAS
wamekutana jana katika Kampasi ya Muhimbili (MUHAS), ili kuangalia dhana
mpya kwa ajili ya utoaji huduma za afya kwa njia ya mtandao katika
kijiji cha Wamasai, Mkoani Arusha cha Ololosokwan. Mwakilishi
wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO),
Zulmira Rodrigues akizungumza katika warsha ya siku mbili ya kujadili
na kuiangalia dhana ya tiba mtandao na namna ya kuitekeleza inayoendelea
jijini Dar Es SalaamKijiji hicho tayari kina uwezo wa kupata huduma hizo. Mradi huo ukifanikiwa unatarajiwa kupanuliwa kwenda sehemu mbalimbali
zinazohitaji matibabu ya mabingwa lakini uwezo wa kufika huko haupo. “Dhana hii itawezesha kuendelea na utoaji wa huduma bora
za afya, zenye ufanisi wa kitaalamu zaidi katika maeneo ya vijijini,
ambayo mara nyingi huachwa nyuma katika utoaji wa huduma hizo,”alisema
Zulmira na kuongeza kuwa dhana ya utabibu mtandao inalenga hasa kuinua
utumiaji wa teknolojia ya kidigitali ya kisasa, ambapo utekelezaji wake
utakuwa mfano elekezi wa kuboresha matumizi ya teknologia katika karne
ya ishirini na moja katika utoaji wa huduma za afya nchini na barani
Afrika. Makamu
Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT), Prof. Elifas Bisanda akitoa
neno katika warsha ya siku mbili ya kujadili na kuiangalia dhana ya tiba
mtandao na namna ya kuitekeleza inayoendelea katika ukumbi wa MUHAS
jijini Dar Es Salaam.Warsha inayochambua dhana ya tiba mtandao ni awamu ya pili yenye
kuendeleza juhudi za kutumia uwapo wa huduma hiyo Ololosokwan kwa
kuwakutanisha wabunifu, wataalamu wa afya na wanateknolojia ili
kudadavua dhana ya utekelezaji kamilifu wa jaribio la utoaji wa huduma
za afya kwa kutumia teknolojia ya kisasa, na baadaye kuirasimisha kama
mfumo wa kuboresha afya maeneo yaliyo pembezoni ya miji na vijijini. Katika warsha hiyo washiriki walipata nafasi ya kushuhudia utiaji
saini wa makubaliano kati ya Unesco na MUHAS wa ushirikiano katika
utekelezaji wa dhana hiyo ya tiba mtandao. Akifafanua zaidi Dk Vumilia alisema kwamba tiba mtandao itahusisha
upasuaji mdogo ambao utafanywa na wataalamu waliopo katika kliniki za
kijiji hicho wakielekezwa na mtaalamu bingwa. Mwakilishi
wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO),
Zulmira Rodrigues akifuatilia kwa umakini hotuba mbalimbali
zilizowasilishwa kwenye warsha hiyo.Meneja
Mradi wa Kijiji cha Kidigitali kutoka UNESCO, Tiina Neuvonen akifafanua
jambo kwenye warsha ya siku mbili ya kujadili na kuiangalia dhana ya
tiba mtandao na namna ya kuitekeleza inayoendelea katika Chuo Kikuu cha
Afya na Sayansi-Muhimbili (MUHAS) jijini Dar es Salaam.Mwakilishi
wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO),
Zulmira Rodrigues (kushoto) pamoja na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu
cha Afya na Sayansi-Muhimbili (MUHAS), Prof Eligius Lyamuya wakitiliana
saini mkataba wa makubaliano ya kurasimisha ushirikiano wao katika
uendeshwaji wa mradi mzima wa Kijiji cha Uvumbuzi wa Dijitali ya Afya.
Wanaoshuhudia tukio hilo waliosimama ni Mratibu wa E-Medicine kutoka
Idara ya Tiba Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, Dr. Liggy Vumilia (kushoto) na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria
Tanzania (OUT), Prof. Elifas Bisanda (kulia).Mwakilishi
wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO),
Zulmira Rodrigues, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na
Sayansi-Muhimbili (MUHAS), Prof Eligius Lyamuya na Makamu Mkuu wa Chuo
Kikuu Huria Tanzania (OUT), Prof. Elifas Bisanda wakishuhudia Mratibu wa
E-Medicine kutoka Idara ya Tiba Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto, Dr. Liggy Vumilia (kushoto) akiweka saini kama
shahidi wa makubaliano hayo.Mwakilishi
wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO),
Zulmira Rodrigues na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na
Sayansi-Muhimbili (MUHAS), Prof Eligius Lyamuya wakibadilishana hati za
mkataba wa makubaliano ya kurasimisha ushirikiano wao katika uendeshwaji
wa mradi mzima wa Kijiji cha Uvumbuzi wa Dijitali ya Afya huku tukio
hilo likishuhudiwa na wataalamu kutoka Shirika la Afya Duniani,
Mwakilishi wa Tamisemi, Wizara ya Afya, DMO wa Ngorongoro, wataalamu
kutoka KCMC na MUHAS. Picha
juu na chini ni wataalamu kutoka KCMC, MUHAS wadau kutoka The Africa
Foundation, Aga Khan Foundation, Ubalozi wa Uswisi, Bill & Melinda
Gates Foundation, pamoja na Maafisa wa Afya wa mikoa na wilaya za Arusha
na Ngorongoro wanaoshiriki warsha ya siku mbili ya kujadili na
kuiangalia dhana ya tiba mtandao na namna ya kuitekeleza. Katibu
Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk
Mpoki Ulisubisya (kulia) akibadilishana mawazo na Mganga Mkuu wa Wilaya
Ngorongoro, Dk. Omari Sukari wakati wa warsha ya siku mbili ya kujadili
na kuiangalia dhana ya tiba mtandao na namna ya kuitekeleza inayoendelea
katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi-Muhimbili (MUHAS)
jijini Dar Es Salaam. Katikati ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha
Afya na Sayansi-Muhimbili (MUHAS), Prof Eligius Lyamuya.Picha ya pamoja.
No comments:
Post a Comment