Rais Donald Trump
amemfuta kazi mkurugenzi wa shirika la ujasusi la FBI kutokana na hatua
yake ya kuliangazia swala la barua pepe za aliyekuwa mgombea wa uraisi
wa chama cha Democrat Hillary Clinton, mamlaka imesema.
Ikulu ya Whitehouse iliishangaza Washington kwa kutangaza kwamba James Comey amefipigwa kalamu. Lakini wanachama wa Democrats wamesema kuwa alifutwa kazi kwa sababu FBI ilikuwa ikuchunguza madai ya uhusiano kati ya Trump na Urusi.
Hatua hiyo inajiri baada ya kubainika kwamba bwana Comey alitoa habari za uongo kuhusu barua pepe za Clinton kwa bunge la Congress wiki iliopita.
- Trump amfuta kazi mkurugenzi wa FBI James Comey
- Clinton alaumu FBI kwa kushindwa kwake
- FBI imethibitisha kuichunguza Urusi
Bwana Sessions alisema kuwa idara ya haki ina nidhamu ya hali ya juu, uadilifu na sheria na mwanzo mpya unahitajika.
Ikulu ya Whitehouse imesema kuwa utafutaji wa mrithi wake unaanza mara moja.
Naye kiongozi wa chama cha Democratic katika Bunge la Seneti, Bwana Chuck Schumer, amesema kuwa ni wakati mwafaka sasa kumteua kiongozi maalumu wa mashtaka kusimamia uchunguzi huo juu ya uhusiano na Urusi.
- FBI: Clinton hana shitaka la kujibu
- Mkurugenzi wa FBI apinga madai ya Trump kuhusu Obama
- Trump alalamika FBI kumuondolea makosa Clinton
Ikulu ya White House imekanusha kuwa kutimuliwa kazini kwa Bwana Comey kuna uhusiano wowote na maswala ya kisiasa.
CHANZO: BBC
SHARE
No comments:
Post a Comment