Rais wa Marekani
Donald Trump anatarajiwa kukutana na kiongozi wa utawala wa palestina
Mahmoud Abbas wakati wa siku ya pili ya ziara yake Mashariki ya Kati
Waisrael na wapalestina hawajafanya mazungumzo ya moja kwa moja kwa zaidi ya miaka mitatu. Waandamanaji walirusha mawe kupinga ziara ya Trump huko Ukingo wa Magharibi siku ya Jumatatu
- Trump anajali amani ya Israel na Palestina?
- UN yamuonya Trump kwa msimamo kuhusu Israel na Palestina
Pia alionya juu ya kuwepo kwa tisho la Iran kwa amani ya dunia
Ziara huiyo ya siku mbili nchini Israel na katika utawala wa Palestina ni sehemu ya ziara ya ya kwanza ya kigeni ya bwana Trump.
Rais Trump anajitambua kama mpatanishi mkuu wa kutatua masuala ambayo yamewashinda watu wengi.
Suala kuu ni kubuniwa kwa taifa huru la palestina kando ya Israel.
Baadhi ya watu wenye ushawishi ndani ya serikali ya Israel wanaamini kuwa ardhi hiyo ni ya Waisraeli waliyopewa na Mungu.
Utawala wa Palestina umegawanyika huku Kundi la Fatah likitawala huko Ukingo wa Magharibi na Hamas huko Gaza.
SHARE









No comments:
Post a Comment