Uingereza
itasambaza wanajeshi kwa ajili ya kulinda maeneo muhimu na kwenye
matukio mbalimbali, kufuatia shambulio la kigaidi lililotokea katika mji
wa Manchester na kusababisha vifo vya watu 22.
Hatua hiyo isiyo
ya kawaida imetangazwa na Waziri mkuu wa nchi hiyo Theresa May, ambaye
amesema ukadiriaji unaofanywa juu ya kitisho cha ugaidi kinachoikabili
nchi hiyo, umeongezwa kwa kiwango kikubwa.Ikiwa na maana kwamba mashambulio ya kigaidi yanaweza kutokea tena.
Waziri mkuu wa Uingereza amesisitiza kuwa kuna uwezekano wa kundi la watu lina weza kuwa na uhusiano na shambulio la Jumatatu usiku la Manchester.
CHANZO: BBC
SHARE
No comments:
Post a Comment