Usimamizi usiofaa wa miradi mbalimbali ya maji nchini umeelezwa kuwa ni kikwazo kwa juhudi za kuwezesha upatikanaji wa maji kwa kila familia.
Hayo yalisemwa jana na Mkurugenzi Msaidizi Wizara ya Maji na Umwagiliaji Injinia Jackson Mutazamba katika semina ya inayofanyika mjini Morogoro ikijuimuisha wakurugenzi kutoka halmashauri zote nchini.
Alisema lengo la semina hiyo ni kuweza kuwahimiza na kuwajengea uelewa zaidi wakurugenzi hawa namna ya kufanya miradi ya maji iweze kuwa na tija na kufanya upatikanaji wa maji kwa wananchi isiwe kikwazo.
"Utawala bora katika usimamizi wa miradi ya maji ni kitu cha msingi sana katika kufanya miradi ya maji iwe endelevu mara baada ya kuanzishwa na kuweza kuwapatia wananchi maji wakati wote wa mwaka," alisema.
Alisema hadi mwezi wa tatu mwaka huu mtandao wa maji ulikuwa umefikia asilimia 72 nchini pote lakini miradi mingine haifanyi kazi kutokana na utawala mbovu hivyo kufanya kuwe na upungufu mkubwa wa maji.
Alisema wakurugenzi wa wilaya ni viungo muhimu sana katika kufanya miradi hii ya maji iwe endelevu ukizingatia kuwa serikali na wadau wa maendeleo wamekuwa karibu sana katika kuhakikisha miradi mingi ya maji inaanzishwa.
Pia wakurugenzi wanaweza kusimamia uanzishwaji wa kamati maalumu za maji ambazo zinasimamiwa moja kwa moja na wananchi wenyewe hivyo kufanya miradi hii iwe endelevu.
Akiwasilisha makadirio ya bajeti kwa mwaka 2017/18 bungeni Dodoma wiki iliyopita, Waziri wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Injinia Gerson Lwenge alisema serikali imejipanga kuanzisha miradi mipya mingi ili kuweza kuongeza mtandao wa maji kufikia asilimia 95.
Mkurugenzi wa halmashauri ya mpanda Rojas John Lomuli akiahidi kuitikia wito wa kuendeleza usafi wa mazingira ili kuhakikisha halamashauri yake inafikia kiwango cha juu katika utekelezaji wa kampeni ya Nipo Tayari iliyowashirikisha wakurugenzi wa halmashauri nchini kuhusu skimu ya malipo kwa matokeo inayofanyika mjini morogoro
Mkurugenzi wa halmashauri ya kondoa Khalifa Kondo akionyesha ishara ya kampeni ya Nipo Tayari ya kutekeleza usafi wa mazingira katika mji wake wakati wa semina ya kwa wakurungenzi wa halamashauri nchini kuhusu skimu ya malipo kwa matokeo inayofanyika mjini morogoro.
Mkurugenzi wa halmashauri ya Ikungi mkoani Singida Rustika Turuka akielezea matarajio yake wakati wa semina ya utekerezaji wa kampeni ya Nipo Tayari iliyowashirikisha wakurugenzi wa halmashauri nchini kuhusu skimu ya malipo kwa matokeo, inayofanyika mjini Morogoro
SHARE
No comments:
Post a Comment