TRA

TRA

Tuesday, May 30, 2017

WATANZANIA WAISAIDIE SERIKALI KATIKA KUTATUA CHANGAMOTO SEKTA MBALIMBALI-BONIFACE

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


Watanzania wameaswa kuisaidia serikali katika kutatua changamoto katika sekta mbalimbali ili kujiletea maendeleo kwa haraka, badala ya kusubiri kila jambo lifanywe na serikali.

Kauli hiyo imetolewa na Mdau wa maendeleo Boniface Myalla wakati alipotembelea shule ya Msingi Kunguru iliyopo Goba na kugawa Daftari kwa wanafunzi 300 wa darasa la kwanza.

Mayala amesema, Watanzania hawana budi kuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali inayoongozwa na Rais Dk.John Pombe Magufuli za kuhakikisha inaleta maendeleo na huduma bora kwa wananchi.

"Serikali imetekeleza jukumu lake la kutoa elimu bure, imekuwa ikitoa fedha kwa ajili ya wanafunzi kusoma bure, sasa imebaki upande wetu wazazi na walezi kuwawezesha wanafunzi kupata vifaasaidizi," amesema.

Amesema lengo la kutoa madaftari hayo ni kuunga mkono serikali ya Rais Dk. John Pombe Magufuli katika dhamira yake ya kuhakikisha Tanzania mpya inajengeka, Tanzania ambayo kila Mtanzania atanufaika na nchi yake lakini pia kupata elimu bora.

Akizungumza baada ya kupokea zawadi hizo, Mwalimu wa wanafunzi hao, Sikujua Ramadhani amemshukuru Myala na kuiomba serikali na wadau wengine kujitokeza na kutoa msaada ili kukamilisha malebgo na ndoto za wanafunzi. Amesema wapo wanafunzi walikjuwa wakishindwa kuandika kwa kukosa madaftari na vifaa vingine vya kujifunzia hivyo ujio wa madaftari hayo utapunguza kero changamoto hiyo.


Mdau wa maendeleo Boniface Myala akizungumza na wanafunzi alipotembelea shule ya Msingi Kunguru Goba na kugawa madaftari kwa wanafunzi 300 wa darasa la kwanza leo jijini Dar es Salaam.
Mdau wa maendeleo Boniface Myala akikabidhi daftari kwa Mwalimu wa wanafunzi hao, Sikujua Ramadhani leo jijini Dar es Salaam.(picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii)
Mdau wa maendeleo Boniface Myala akigawa daftari kwa wanafunzi wa darasa la kwanza wa shule ya Msingi Kunguru Goba . Leo jijini Dar es Salaam.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger