Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe
(katikati) akifafanua jambo wakati wa kikao na uongozi wa Klabu ya
michezo ya Afrika Lyon katika ukumbi wa Idara ya Habari maelezo leo
Jijini Dar es Salaam, kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari
(MAELEZO) Bw. Patrick Kipangula na kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Klabu ya
afrika Lyon Bw.Rajuu Kagenzi.
Mtendaji
Mkuu wa Klabu ya afrika Lyon Bw.Rajuu Kagenzi (kushoto) akiongea wakati
wa kikao na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison
Mwakyembe (katikati) na kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari
(MAELEZO) Bw. Patrick Kipangula .
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia)
akipokea jezi kwa niaba ya Rais Dkt.John Pombe Magufuli kutoka kwa
Mtendaji Mkuu wa Klabu ya afrika Lyon Bw.Rajuu Kagenzi (kushoto) mara
baada ya kikao na uongozi huo leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia)
akionyeshwa michora ya ramani za viwanja vya michezo vinavyotarajiwa
kujengwa kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya afrika Lyon Bw.Rajuu
Kagenzi (kushoto) leo Jijini dar es Salaam.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe
(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa uongozi wa Klabu
ya michezo ya Afrika Lyon katika ukumbi wa Idara ya Habari maelezo leo
Jijini Dar es Salaam. (Picha na Lorietha Laurence-WHUSM)
Na Lorietha Laurence
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe
ameupongeza uongozi wa Klabu ya michezo ya Afrika Lyon kwa kutumia
mchezo wa mpira wa miguu kuelimisha jamii kupambana na ujangili wa
tembo.
Waziri
Mwakyembe ametoa pongezi hizo leo Jijini Dar es Salaam wakati
alipokutana na uongozi wa klabu hiyo katika kikao kilichofanyika katika
ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO.
Katika
kikao hicho uongozi wa timu hiyo ulimueleza Waziri kuwa timu yao
imeamua kushiriki vita dhidi ya vitendo vya mauaji ya tembo kwa kuandika
ujumbe maalum katika jezi za timu hiyo kuelimisha jamii dhidi ya
vitendo hivyo.
“ni
jambo zuri kuhakikisha jamii inapata burudani ya mpira wakati huo huo
inaelimika kupitia ujumbe unatolewa na wachezaji katika jezi zao”Dkt
Mwakyembe alisema.
Kwa hivyo, aliushukuru uongozi wa timu hiyo kwa juhudi zao hizo na kukieleza kitendo hicho kuwa ni “cha mfano na kujivunia”.
Aliongeza
kuwa Serikali inajivunia na kuthamini mchango wa wananchi wazalendo
wanaojitolea kujenga taifa na kulinda rasilimali zake kama timu
ilivyofanya timu hiyo.
Aidha
Waziri Dkt. Mwakyembe aliongeza kuwa ni jambo jema linalofanywa na
klabu hiyo katika kuhakikisha inakuza na kuendeleza vipaji kwa vijana
mbalimbali nchini jambo ambalo linasaidia kuinua sekta ya michezo.
Pia
aliwapongeza kwa kupata fursa ya kutembelea nchi ya China kwa ajili ya
kujifunza mambo mbalimbali yanayohusu michezo na kuwataka kuitumia fursa
hiyo ipasavyo kwa kujifunza kwa bidii ili watakaporejea waweze
kufundisha vijana wengine wa kitanzania.
Naye
Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Afrika Lyon Bw. Rajuu Kangezi ameeleza kuwa
mkakati wa klabu hiyo ni kuhakikisha kuwa inajenga viwanja vya michezo
vya kisasa kwa matumizi ya jamii ili kuendeleza michezo nchini hivyo
ameomba ushirikiano na serikali katika kufanikisha mikakati hiyo.
“Tuna
mipango mingi ya kuhakikisha tunakuwa na viwanja vizuri vya michezo na
hili haliwezi kufanikiwa bila kuishirikisha serikali na viongozi wake
hivyo tunaomba ushirikiano wa serikali katika kuhakikisha tunafanikisha
jambo hili”
Katika
kikao hicho uongozi wa klabu hiyo ulimkabidhi Waziri Mwakyembe jezi
namba tano “5” ya klabu hiyo kwa ajili ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
SHARE
No comments:
Post a Comment