Aliyekuwa rais wa
Gambia Yahya Jammeh aliiba takriban dola milioni 50 kutoka kwa taifa
kabla ya kuondoka nchini humo mwezi Januari, kwa mujibu wa waziri wa
sheria.
Kwa sasa mahakama imeagiza kutwaliwa kwa mali yake yote yaliyosalia nchini Gambia.
Jammeh alikimbia kuenda nchini Equitorial Guinea baada ya miaka 22 uongozini.
Jammeh alikimbia kuenda Equitorial Guinea baada ya miaka 22 uongozini.
Magari ya kifahari na bidhaa zingine ziliripotiwa kuingiza kwenye ndege ya mizgo ya Chad wakati Jammeh alikuwa akiondoka nchini humo.
Pesa hizo zilitajwa kuwa dola milioni 11 na waziri wa masuala ya ndani Mai Ahmad Fatty, ambaye wakati huo alikuwa msaidizi wa rais Adama Barrow.
Lakini siku ya Jumatatu waziri wa sheria Abubacarr Tambadou, alisema kuwa bwana Jammeh aliiba dola milioni 50 kati ya mwaka 2006 na 2016.
CHANZO: BBC
SHARE









No comments:
Post a Comment