Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando (katikati) akitoa ufafanuzi juu ya vocha mpya ya Airtel
Tabasamu ambayo ni maalumu kwa wateja wake wa malipo ya awali
nchini. Kushoto ni Meneja wa chapa wa Airtel , Arnold Madale na Meneja
Masoko ya Airtel, Anethy Muga (kulia). Vocha hiyo itapatikana kuanzia
sasa kupitia maduka yote ya Airtel , wakala na
wachuuzi wa vocha za Airtel nchi nzima.
Kampuni
ya simu za mkononi ya Airtel leo imezindua vocha mpya ya muda wa
maongezi kwa wateja wake wa malipo ya awali nchini itakayowaongezea
wateja wake TABASAMU pale wanapopiga
simu au kuitumia kwa matumizi yoyote ya kuwasiliana au kujiunganisha
kwenye vifurushi vya gharama nafuu.
Vocha hiyo mpya ya
TABASAMU kwa shilingi
200 inapatikana kwa wachuuzi wote wa vocha za Airtel na kuwawezesha
wateja wa Airtel na watanzania wote watakaojiunga na Airtel kumudu
gharama za mawasiliano wakati wowote kwa gharama nafuu zaidi
Akiongea
wakati wa uzinduzi, Meneja Masoko wa Airtel, Bi Aneth Muga alisema,“ Leo tunajisikia fahari kuzindua na kuitambulisha sokoni vocha ya muda
wa maongezi ya shilingi
200 itakayowapatia wateja Tabasamu na uhuru wa kuwasiliana na ndugu
jamaa marafiki au wale wajasiliamali kuweza kuitumia kupanga mipango yao
wakati wowote mahali popote kwa gharama nafuu”
“Tunatambua
mawasiliano ya simu ni muhimu katika kuendesha shughuli zetu za kila
siku na hivyo kuboreshwa kwa viwango vya vocha kutasaidia sana
kuchochea upatikanaji
wa huduma ya mawasiliano kwa wote. Tunataka kuendelea kutoa huduma bora
za kibunifu na zenye kukidhi mahitaji ya wateja wetu huku tukiwawezesha
kutatua changamoto zao za kila siku”. alieleza Muga.
“Tunaamini
kwa kuwezesha upatikanaji wa vocha za shilingi 200 sokoni tumewawezesha
zaidi ya watanzania milioni 10 kuunganishwa na huduma za mawasiliano na
kufurahia
ofa mbalimbal zinazotolewa na Airtel," aliongeza.
Ili kuingia vocha ya muda wa maongezi mteja atapiga
*104*
kisha kuingiza namba zilizokwanguliwa na kubonyesha alama ya reli # na
kisha OK. Vocha hiyo itaingia moja kwa moja kwenye Salio lake la kupiga
simu na mteja ataamua kuitumia kwa kupiga simu au kujiunga na
kifurushi cha shilingi 200 kwa kupiga *149*99#.
SHARE
No comments:
Post a Comment