Katibu Mkuu wa Baraza
la Wazee wa Yanga, Ibrahimu Akilimali ametangaza kuwania nafasi ya
uenyekiti wa klabu hiyo iliyoachwa wazi hivi karibuni na aliyekuwa
mwenyekiti wake, Yusuf Manji.
Hivi karibuni Manji
alitangaza kujiuzulu kwenye nafasi yake hiyo ili aweze kupumzika
kutokana na matatizo mbalimbali aliyokumbana nayo siku chache
zilizopotia.
Lakini pia maamuzi
hayo ya Manji yalikuja ikiwa ni muda mfupi tu umepita tangu
alipotangaza kutaka kuikodi timu hiyo kwa muda wa miaka 10, lakini
akakukumbana na changamoto kibao kutoka kwa baadhi ya wanachama wa klabu
hiyo na kuamua kusitisha mpango wake huo.
Akilimali alisema
anaamini amefikia uamuzi huo ili aweze kuleta mabadiliko makubwa ya
ndani ya klabu hiyo kuanzia pale Manji alipoishia.
Alisema licha ya
kutokuwa bilionea kama ilivyokuwa kwa Manji lakini anaamini kwa kutumia
utajiri wake wa hekima na busara alizonazo ataiongoza klabu hiyo kwa
mafanikio makubwa, kwa hiyo amewataka wanachama kutulia.
"Manji keshaondoka
Yanga akapumzike kutokana na matatizo yaliyompata hivi karibuni kwa hiyo
siyo vizuri kuanza kuumiza vichwa kuwa mambo yatakuaje bila ya yeye.
"Yanga ni timu kubwa,
jina lake na nembo yake tu chanzo kikubwa cha kuingizia mapato endapo
atapatikana kiongozi mwenye uchungu na maendeleo ya Yanga na asiwe
mpigaji.
"Kwa hiyo, katika
uchaguzi ujao ambao utafanyika ili kuziba nafasi iliyoachwa na Manji,
nitagombea nafasi hiyo kwani uwezo wa kuipa Yanga mafanikio ninao,”
alisema.
SHARE
No comments:
Post a Comment