Na Rhoda James
Leo Juni 23, 2017 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na
Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo amekutana na Watendaji kutoka
Benki ya Dunia (WB) waliomtembelea kwa ajili ya kupata taarifa ya
maendeleo ya miradi mbalimbali ya madini inayotekelezwa na Wizara. Kati
ya masuala yaliyojadiliwa ni pamoja na uimarishaji wa Sekta ya Madini,
Mafanikio ya miradi yake pamoja na taasisi.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Nishati na Madini, Dkt. Juliana Pallangyo (mbele) akielezea miradi ya
Sekta ya Madini na mafanikio yake. Wengine katika Picha ni Ujumbe kutoka
Benki ya Dunia (WB), Viongozi Waandamizi kutoka Wizara ya Nishati na
Madini, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mamlaka ya Udhibiti wa
Huduma za Nishati na Maji (EWURA) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).
Watendaji kutoka Wizara ya
Nishati na Madini, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mamlaka ya
Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) na Wakala wa Nishati
Vijijini (REA) wakiwa katika kikao hicho.
Mwakilishi kutoka Benki ya Dunia
Sudeshna Banerjee ( wa kwanza kulia) akielezea mipango walionayo katika
kusaidia utekelezaji wa Miradi ya Sekta ya Madini ili iendane na
Vipaumbele vya Serikali.
SHARE
No comments:
Post a Comment