Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akiwa na
Mbunge wa Tarime mjini Esther Matiko (Chadema) katika uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Dulles Washington DC nchini Marekani ,wakiwa wanarejea
nchini kutoka Marekani walikokuwa wakihudhuria mkutano wa kimataifa
uliowajumuisha viongozi mbalimbali wa nchi wanachama wa Benki ya
Dunia na na IMF, asasi za kiraia, mashirika binafsi kuzungumzia masuala
ya mbalimbali has afya na elimu. Tayari viongozi hao wamewasili nchini
na wanaendelea na majukumu yao
Mkutano huo umeazimia nchi na mashirika
mbalimbali kuwekeza kwenye Lishe ili mataifa kuepuka kuwa na watu
wenye udumavu na hivyo kuathiri uchumi wa nchi.
SHARE
No comments:
Post a Comment