District Governor Mteule, Sharmila Bhatt akimpa muhtasari Rais Mteule wa Rotary International, Barry Rassin (kulia) alipowasili Uwanja wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam Februari 5 2018, kwa ziara ya siku mbili kutembelea miradi mbalimbali ya Rotary Clubs jijini. Rais huyo atatembelea mradi wa 'Rotary Pediatric Oncology wodi iliyopo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, pia kupanda mti katika viwanja vya shule ya wasichana ya Jangwani hapo kwa lengo kuunga mkono mapinduzi ya kijani na utunzaji wa mazingira. Pamoja nao ni District Governor, Bwana Kenneth Mugisha. |
Baadhi ya viongozi wa Rotary Club wakiwa Uwanja wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam Februari 5 2018, wakati wa kumpokea Rais Mteule wa Rotary International Bary Rassin kwa ziara ya siku mbili kutembelea miradi mbalimbali ya Rotary Clubs jijini. Rais huyo atatembelea mradi wa 'Rotary Pediatric Oncology wodi iliyopo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, pia kupanda mti katika viwanja vya shule ya wasichana ya Jangwani hapo kwa lengo kuunga mkono mapinduzi ya kijani na utunzaji wa mazingira. |
Rais Mteule wa Rotary International, Barry Rassin (kulia) akikaribishwa Past District Governor Jayesh Asher alipowasili Uwanja wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam Februari 5 2018, kwa ziara ya siku mbili kutembelea miradi mbalimbali ya Rotary Clubs jijini. Rais huyo atatembelea mradi wa 'Rotary Pediatric Oncology wodi iliyopo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, pia kupanda mti katika viwanja vya shule ya wasichana ya Jangwani hapo kwa lengo kuunga mkono mapinduzi ya kijani na utunzaji wa mazingira. |
RAIS
Mteule wa Rotary International, Barry Rassin (wa sita kulia) na mkewe
Esther (kulia kwake) wakiwa katika picha ya pamoja na District Governor
aliyemaliza muda wake, Bwana Kenneth Mugisha (wa nne kushoto),
District Governor Mtarajiwa, Sharmila Bhatt (wa tano kulia) pamoja na
viongozi mbalimbali wa baada ya kuwasili Uwanja wa kimataifa wa Julius
Nyerere (JNIA) Dar es Salaam, kwa ziara ya siku mbili kutembelea miradi
mbalimbali ya Rotary Clubs jijini.
|
Na Mwandishi wetu
RAIS
Mteule wa Rotary International, Barry Rassin amewasili nchini Tanzania
jana na kulakiwa na wenyeji wake District Governor, Bwana Kenneth
Mugisha, District Governor Mteule, Sharmila Bhatt pamoja na viongozi
mbalimbali wa baada ya kuwasili Uwanja wa kimataifa wa Julius Nyerere
(JNIA) Dar es Salaam, kwa ziara ya siku mbili kutembelea miradi
mbalimbali ya Rotary Clubs jijini.
Rais
huyo aliyetumikia Rotary Club kwa Takribani Miaka 37 amewasili na
kujionea baadhi ya miradi inayofadhiliwa na Taasisi hiyo hapa nchini
hususani kwa jiji la Dar es Salaam, ambapo atakutana na vijana wadogo wa
Club hiyo' Rotaractors' na kubadilishana nao mawazo kuwahamasisha
kujitolea na kufanya shuguli mbalimbali za kijamii ili kuleta maendeleo
chanya kwa umma.
Rotary Club ina takribani matawi 38 ambapo nane kati ya hayo yapo Dar es Salaam.
SHARE
No comments:
Post a Comment