TRA

TRA

Tuesday, June 13, 2017

Halotel yashusha Neema kwa wateja wake

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


Naibu Mkurugenzi wa Halotel, Nguyen Van Son akiweka laini ya simu ya Halotel kwa mteja mpya wa mtandao huo, Salim Selemani, ambaye amejiunga na  wakati wa uzinduzi wa kampeni ya “Switch to Halotel” yenye lengo la kuwahamasisha Watanzania kujiunga na mtandao huo. Kampeni hiyo pia itahusisha wafanyakazi wa halotel kutembelea maeneo mbalimbali na kutoa huduma kwa wateja katika maeneo yao. Pamoja naye katika picha ni Meneja Miradi wa Kampuni hiyo, Frank Mwakyoma na waendesha pikipiki wa kituo cha Makumbusho.

Kampuni ya mawasiliano ya simu ya Halotel, imezindua kampeni mpya ya Switch to Halotel, yenye lengo la kuwahamasisha Watanzania kujiunga na Mtandao huo sambamba na kuzindua utaratibu wa wafanyakazi wa kampuni hiyo kuwatembelea wateja wa Mtandao huo katika maeneo yote nchi nzima mjini na vijijini.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni hiyo iliyofanyika katika soko la Makumbusho lililoko Kinondoni Dar es Salaam, Naibu Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Nguyen Van Son, amesema tangu kuzinduliwa kwa huduma za kampuni hiyo, wamepata mapokezi mazuri kutoka kwa watanzania ambao hadi sasa zaidi ya wateja milioni tatu na laki tano, tayari wamejiunga na mtandao huo na wanafurahia huduma mbalimbali zinazotolewa na kampuni hiyo ya simu.

“Tunafarijika sana kwa namna ambavyo Watanzania wameendelea kutuunga mkono katika jitihada zetu za kuboresha huduma za mawasiliano kwa jamii hii, ni faraja kubwa kwetu kwamba katika kipindi hiki kifupi tumepata mafanikio makubwa na bado tunaendelea kupata wateja wanaojiunga na mtandao wetu siku hadi siku,” Jambo hili linatufanya tusilale tufikilie ni namna gani tunapaswa kuendelea kukizi mahitaji yao.

“Kuzinduliwa kwa kampeni hii itakuwa ni sehemu ya sisi kusogea karibu na wateja wetu, kuwahudumia pamoja na kuwasikiliza ni nini wanahitaji kutoka kwetu,” Tunaamini kabisa kwamba kuwa karibu na wateja wetu tutajenga mtandao bora kabisa utakao kuwa na huduma zinazolenga maisha halisi ya Watanzania.

Aidha Naibu Mkurugenzi huyo alitaarifu kuwa, Kampuni hiyo imeanza utaratibu wa kuwa na vifurushi Maalumu kulingana na maeneo na mahitaji ya wateja husika, Huku akitolea mfano wa kuwa na vifurushi maalumu kwa wateja wa Mtandao huo wa Zanzibar ambao wameanzishiwa kifurushi maalumu cha ZANZIBAR YETU, ambacho kwa watumiaji wa Halotel wataweza kuongea bure siku za mwisho wa wiki kwa shilingi 1000 pamoja na vifurushi vingine, Kwa wateja wapya wa mikoa ya Mbeya, Manyara, Pwani, Arusha, Kilimanjaro na Mara, Mkoa huo wanaweza kupata dakika 60 za kupiga simu bure ndani ya mtandao kila wanapoweka muda wa maongezi kwa siku 30 baada ya kusajili . Pamoja na Ofa ya Kiboko yao ambayo inapatika katika baadhi ya minara ya 3G ya mtandao huo.

Naibu Mkurugenzi huyo alibainisha kuwa, licha ya kuboresha na kutoa huduma zinazowalenga Watanzania, kampuni hiyo pia imeendelea kufanya uwekezaji mkubwa katika kuboresha Mawasiliano na ubora wa Mtandao huo ambapo hivi karibuni mtandao huo ulitangaza uwekezaji wa zaidi ya bilioni 200 kwa ajiri ya kuboresha ubora wa sauti na kasi ya intaneti, huku wakitarajia kuwekeza zaidi katika mwaka ujao wa fedha.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger