Mwanamitindo maarufu nchini,
Jokate Mwegelo akikabidhi misaada kwa Mwenyekiti wa Taasisi
inayoshughulikia masuala mbalimbali ya Wajane na Watoto Yatima
ijulikanayo kwa jina la Ahbaabul Khairiya, Ahmed Chebe ya Mwanayamala B
jijini Dar es Salaam. Jokate ambaye pia ni Kaimu Katibu Hamasa na
Chipukizi wa Umoja wa Vijana Tanzania (UVCCM) amebidhi kilo 250 za unga
na mchele, mbuzi wawili, mafuta ya kupikia, nguo za watoto wa kike na wa
kiume, mafuta yakupikia na nguo za watu wazima kwa ajili ya
kusheherekea sikukuu ya Eid El Fitr kwa faraja zaidi.
Mmoja wa wajane wa Taasisi ya
Ahbaabul Khairiya, Nawili Saidi akibeba nguo mbalimbali zilizotolewa na
Mwanamitindo, Jokate Mwegelo kwa ajili ya kusheherekea sikukuu ya Eid El
Fitr.
Jokate akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa kituo cha Ahbaabul Khairiya pamoja na wajane na yatima.
Wanawake wajane wakimshukuru Jokate mara baada ya kutoa msaada katika kituo hicho.
…………………..
Mwanamitindo, Miss Tanzania namba
mbili 2006 na mbunifu wa mavazi, Jokate Mwegelo ametoa sadaka ya sikukuu
ya Eid El Fitr kwa taasisi ya wanawake wajane na watoto yatima
ilijulikanayo kwa jina la Ahbaabul Khairiya cha Mwanayamala B jijini Dar
es Salaam.
Jokate ametoa zawadi hiyo kwa
kituo hicho chenye jumla ya wajane 32 na watoto yatima 41 kama sehemu ya
kuwafanya wajane na yatima hao kusheherekea sikukuu ya Eid El Fitr kwa
faraja zaidi.
Mrembo huyo ambaye pia ni Kaimu
Katibu Hamasa na Chipukizi wa Umoja wa Vijana Tanzania (UVCCM) amebidhi
kilo 250 za unga na mchele, Mbuzi wawili, mafuta ya kupikia, nguo za
watoto wa kike na wa kiume, mafuta yakupikia na nguo za watu wazima.
Amesema kuwa ameguswa na
changamoto za kituo hicho ambacho kimefanya kazi kubwa kujua changamoto
mbalimbali za wajane na watoto yatima wa mikoa ya Dar es Salaam na
Pwani.
“Nimegushwa sana na kuamua kidogo
nilichonacho kugawana na ninyi, sikukuu ya Eid El Fitr inakaribia na
natarajia kila mmoja wetu atasheherekea kwa faraja zaidi, naomba mpokee
msaada huu na matarajio yangu ni kuendelea kuwasaidia pindi ninapata
nafasi,” alisema Jokate.
Mmoja wa wasanii wa luninga
nchini, Juma Chikoka ambaye alikuwa katika makabidhiano hayo alitoa wito
kwa jamii kuunga mkono juhudi za Jokate za kutatua changamoto
mbalimbali katika jamii.
Mwenyekiti (Amiri) wa Taasisi
hiyo, Ahmed Shebe alimshukuru Jokate kwa msaada huo na kuomba wadau
mbalimbali kujitokeza kutatua changamoto hizo.
“Taasisi inahudumia wajane wa
mikoa ya Pwani na Dar es Salaam, wapo wengine Chalinze na Bagamoyo mbali
ya hapa wa jijini, tunajitahidi kutafuta michango sehemu mbalimbali ili
kuweza kuondoa changamoto hizi, hata hivyo bado hatujafikia lengo,
tunahitaji msaada kwa wasamaria ili kuwapa faraja zaidi,”
“Kuna wajane wanaosaidiwa kulipia
kodi yay a nyumba na watoto yatima wanaolipiwa ada, hatuna uwezo mkubwa
wa kufanya hivyo na zaidi fedha za msaada zinatokana na michango yetu,”
alsema Shebe.
SHARE
No comments:
Post a Comment