Na Mwandishi Wetu, Morogoro
MJASIRIAMALI
mwanamke mwenye umri wa miaka 26, Magreth Sinyangwa amekabidhiwa jumla
ya Sh Milioni 20 za ushindi wa bahati nasibu ya Biko, aliyoupata katika
droo kubwa iliyochezeshwa juzi Jumatano, jijini Dar es Salaam, huku
akiwa mwanamke wa kwanza kuibuka na ushindi huo.
Sinyangwa
amekabidhiwa fedha hizo Kilosa katika benki ya NMB, mkoani Morogoro na
Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, ambaye pamoja na mambo mengine,
alimpongeza mshindi huyo na kumtaka azitumie fedha zake kwa uangalifu
pamoja na kuboresha maisha yake ya kila siku.
Akizungumza
katika makabidhiano hayo, Heaven alisema ni wakati wa kutajirika kwa
kutumia vyema bahati nasibu ya Biko, ‘Ijue Nguvu ya Buku’ iliyozidi
kuchanja mbuga na kutoa mamilioni ya Sh kwa washindi wa droo kubwa
zinazofanyika Jumatano na Jumapili, sanjari na zawadi za papo kwa hapo.
“Tunajivunia
kumpata mshindi mwanamke ambaye leo (jana) tumemkabidhi zawadi yake ya
Sh Milioni 20, tukiamini kuwa atazitumia vizuri katika kuhakikisha
kwamba anakuza biashara zake, ukizingatia kuwa tayari yupo kwenye tasnia
ya biashara kabla ya kupata donge nono la Biko.
“Kucheza
ni rahisi kwa sababu Biko inachezwa kwenye simu za Tigo Pesa, M-Pesa na
Airtel Money, ambapo mtu atafanya muamala kuanzia Sh 1,000 na kuendelea
ambapo ataweka namba ya kampuni ambayo ni 505050 na ile ya kumbukumbu
ni 2456, huku mbali na donge nono la Sh Milioni 20 linatoka kila
Jumatano na Jumapili, pia zipo zawadi za papo hapo kuanzia Sh 5,000,
10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni,” Alisema Heaven.
Naye
Sinyangwa alishindwa kuzuia furaha yake baada ya kukabidhiwa fedha
zake, akisema kuwa ameshukuru ushindi wake huo akisema maisha yake
yatabadilika kwa sababu atatumia biashara zake zipanuke kwa kutumia
vyema ushindi huo wa Biko uliompatia mamilioni ya fedha.
“Huu
ni wakati wa kusonga mbele kiuchumi kwa kutumia fedha hizi ambazo
nimezipata bila kutarajia, hivyo nawaomba akina mama wenzangu pamoja na
Watanzania wote kucheza Biko kwa sababu kila mtu anaweza kushinda bila
kuangalia yupo wapi na anaishi vipi.
“Mimi
nipo Kilosa Morogoro, lakini nilishangaa nilipopigiwa simu na mtu
anayeitwa Kajala Masanja na kuniambia kuwa nimeshinda Biko, lakini nzuri
zaidi leo (jana) wameniletea fedha zangu hadi ninapoishi jambo ambalo
naona si la kawaida na ni la pekee kwa hawa Biko,” Alisema.
Mbali
na kukabidhiwa fedha hizo jumla ya Sh Milioni 20, Biko pia tayari
wametoa zaidi ya Sh Milioni 500 kwa washindi wake walioshinda katika
mwezi Mei pekee, ikiwa ni siku chache tangu kuanzishwa kwa bahati nasibu
hiyo inayotikisa katika kona mbalimbali hapa nchini..
Meneja
Masoko wa Biko, Goodhope Heaven kulia akiwa katika makabidhiano ya Sh
Milioni 20 kwa mshindi wao wa Kilosa, mkoani Morogoro, Magreth Senyangwa
aliyeibuka kidedea katika droo kubwa iliyofanyika Jumatano iliyopita.
Kushoto ni mume wa Magreth, Bahati Ramadhani na mwingine ni Ofisa wa NMB
Tawi la Kilosa, akiwa kwenye makabidhiano hayo.
Mshindi
wa donge nono la Sh Milioni 20 kutoka Kilosa, mkoani Morogoro, Magreth
Senyangwa akiwa ameshika fedha zake baada ya kukabidhiwa kutoka kwa
waendeshaji wa bahati nasibu ya Biko.
SHARE
No comments:
Post a Comment