Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
BENKI
ya CRDB imeadhimisha siku ya Mtoto wa Afrika kwa kuwapatia zawadi
watoto mbalimbali ambao wazazi wao waliwafungulia akaunti za Junior
Jumbo huku wakiwa wamewekewa fedha mara kwa mara.
Akitoa
zawadi hizo, Mkurugenzi wa Tawi la Benki ya CRDB Azikiwe Nomina Msoka
amesema kuwa watoto hao waliopatiwa zawadi ni kutokana na wazazi wao
kuwawekea fedha mara kwa mara na hata akiba za akaunti zao zina kiasi
kikubwa cha fedha.
Nomina
amesema kuwa, wazazi wanatakiwa kuwafungulia na kuwawekea watoto wao
fedha mara kwa mara iili kuwandaa na maisha ya baadae ikiwemo katika
kulipia ada za masomo yao na pia upo taratibu wa wazazi kuwaekea hela
kupitia akaunti zao..
Amesema
mbali na hilo, CRDB wameweza kuandaa michezo mbalimbali ya watoto kwa
ajili ya kujumuika pamoja na wenzao na kufahamiana zaidi.
Mkurugenzi
wa Tawi la Benki ya CRDB Azikiwe Nomina Msoka akiwa amembeba mtoto
Kinora Brown na kumkabidhi zawadi yake ya begi la Junoir Jumbo Akaunti
kwa mama yake wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika
yanayoadhimishwa Juni 16 kila mwaka.
Mkurugenzi wa Tawi la Benki ya CRDB Azikiwe Nomina Msoka akimkabidhi zawadi ya begi la Junoir Jumbo Akaunti mtoto Orley Mwanyika wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yanayoadhimishwa Juni 16 kila mwaka.
Mkurugenzi wa Tawi la Benki ya CRDB Azikiwe Nomina Msoka akimkabidhi zawadi ya begi la Junoir Jumbo Akaunti mtoto Tonia Naivasha wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yanayoadhimishwa Juni 16 kila mwaka.
Mkurugenzi wa Tawi la Benki ya CRDB Azikiwe Nomina Msoka akimkabidhi zawadi ya begi la Junoir Jumbo Akaunti mtoto Rashidi Jumbe wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yanayoadhimishwa Juni 16 kila mwaka.
Mkurugenzi wa Tawi la Benki ya CRDB Azikiwe Nomina Msoka akiwa katika
picha ya pamoja na watoto aliowakabidhi zawadi za mebegi ya Junior Jumbo
Akaunti wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yanayoadhimishwa Juni 16 kila mwaka.
Mkurugenzi wa Tawi la Benki ya CRDB Azikiwe Nomina Msoka akizungumza
na watoto hao baada ya kumalizika kwa zoezi la ugawaji zawadi wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yanayoadhimishwa Juni 16 kila mwaka.
Watoto
waliojitokeza katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika wakiwa
wanacheza michezo mbalimbali iliyoandaliwa na tawi la benki ya CRDB
Azikiwe. Picha zote na Zainab Nyamka.
SHARE
No comments:
Post a Comment