Mataifa yanayozalisha maparachihi kwa wingi zaidi duniani
1. Mexico |
2. Jamhuri ya Dominika |
3. Colombia |
4. Peru |
5. Indonesia |
Wakati hali ikiwa hivyo, wanaume watatu
katika jimbo la California nchini Marekani wamekamatwa na kuzuiliwa,
wakituhumiwa kuiba maparachichi ya thamani ya $300,000 (£234,770) .
Polisi wanasema hilo huenda liliwafanya wanaume hao kushawishika kuiba matunda hayo kutoka kwa kampuni ya matunda ya Oxnard walipokuwa wanafanya kazi.
Afisi ya liwali wa wilaya ya Ventura imesema Carlos Chavez, Rahim Leblanc, na Joseph Valenzuela walikamatwa Jumatano.
Walikuwa wamefanya kazi katika Mission Produce, moja ya kampuni zinazoongoza duniani kwa usambazaji wa maparachichi, kwa miaka kadha.
- Sababu ya ndizi kugeuka rangi na kuivisha matunda mengine
- Matunda na mboga hupunguza hatari ya ugonjwa wa moyo
Rais wa kampuni hiyo, Steve Barnard, anasema sanduku moja ya maparachichi kawaida huuzwa $50, lakini wanaume hao walikuwa wanauza nusu ya bei hiyo.
"Tunachukulia visa kama hivi vya wizi kwa uzito sana. Ni zao muhimu sana hapa na California."
CHANZO: BBC |
---|
SHARE
No comments:
Post a Comment